Tuesday, 24 January 2023

JESHI LA POLISI MKOANI TANGA,LIMEWAASA WAVUVI NA WAFANYABIASHARA WA SAMAKI KUNUSURU MAENEO YALIYOFANYIWA USAFI KUGEUKA MAFICHO YA VIBAKA,,,

Pichani wa pili kutoka mkono wa kushoto ambaye anazoa takataka ni Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe leo asubuhi  akishiriki zoezi la usafi wa mazingira akiwa ameungana na askari pamoja,watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga na watumiaji wa soko hilo.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la polisi Mkoani Tanga  limewaasa wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kutokuwa tayari kuruhusu maeneo yaliyofanyiwa usafi kuwa maficho ya vibaka na watumiaji wa dawa za kulevya. 

ametoa kauli hiyo jana asubuhi (leo) mara baada ya kushiri zoezi la usafi wa mazingira akiwa ameungana na askari pamoja,watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga na watumiaji wa soko hilo.

Mwaibambe alisema kuwa suala la usafi wa mazingira ni lenye kuihusu jamii nzima na ndio maana wamewiwa kushirikiana na wavuvi kufanya usafi kwenye soko hilo la samaki.

Alisema,licha ya ulinzi wa raia na mali zake pia polisi ni miongoni mwa wadau katika utunzaji wa mazingira kwa na zoezi hilo  litakuwa endelevu kufanyika kwa kuhusisha wilaya zote za mkoa wa Tanga kama ambavyo askari wa Tanga Jiji wamefanya.

"Dunia inaharibika tulijisahau tabia za mabadiliko ya nchi imebadilika suala la mazingira ni la wote,hivyo kuna kila sabababu ya polisi kushirikiana na wadau wengene nchini"alisema Kamanda Mwaibambe.

Nae,Nora Makaranga ni Mwenyekiti wa soko la Deep sea, alipongeza ushirikiano uliooneshwa na jeshi la polisi katika kufanya usafi wa mazingira ya eneo hilo.

Alisema kitendo hicho kilichooneshwa na jeshi la polisi kinapaswa kuigwa na watu wengine akiwahimiza wavuvi wenzake kuimarisha usafi wa mazingira.

Naye afisa usafi na mazingira wa Jiji la Tanga,Kizito Nkwabi amelipongeza jeshi la polisi kwa kuandaa tukio hilo muhimu la usafi ambalo linahusisha usalama wa afya za wananchi.

Alisema tayari mpango mkakati umewekwa na halmashauri kuendeleza zoezi la usafi kwa kushirikisha wavuvi,wafanyabiasha na wadau ili kuwezesha kuweka mazingira hayo salama na kuwezesha kuwavutia wafanyabiara wengi.
Mwisho.

Pichani wa pili kutoka mkono wa kushoto ambaye anazoa takataka ni Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe leo asubuhi akiongoza askari zoezi la kufanya usafi wa mazingira akiwa ameungana na watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga na watumiaji wa la Deep sea .


Pichani ni miongoni mwa askari wa jeshi la polisi wa wilaya ya Tanha wakishiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira wakiwa ameungana na watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga na watumiaji wa soko la Deep sea jijini Tanga.











 

No comments:

Post a Comment