Pichani mkono wa kulia ambaye amevaa miwani ni Mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikal WHO IS HUSSEIN FOUNDATION,Azim Dewji akizungumzia lengo la kuandaa zoezi la kuchangia damu kwa jamii na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuweza kuunga mkono ili kuongeza benk ya damu katika hospital ya rufaa Bombo.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TAASISI ya WHO IS HUSSEIN FOUNDATION imefanikiwa kukusanya Unit 419 za damu ili kusaidia wagonjwa wenye uhitaji katika hosptal ya rufaa ya Bombo iliyopo mkoani Tanga.
Mratibu wa huduma za Maabara na damu salama mkoa Tanga,Juma Kayanda ambapo alisema kuwa wamefanikiwa kukusanya uniti hizo 419 za Damu baada ya kuandaa zaoezi la uchangiaji damu kwa jamii liilifanyika viwanja vya Mkwakwani jijini hapo.
Alisema kwamba lengo la zoezi hilo ikiwa ni kuunga mkono Maadhimisho ya miaka 46 tangu kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM.
Aidha,alisema sambamba na maandalizi ya uzinduzi wa uwashaji wa taa katika viwanja hivyo vya Mkwakwani ambapo kuelimisha jamii kujenga utamaduni wa kuchangia damu ili kunusuru vifo vya mama na mtoto.
Akizungumzia zaidi zaidi,Mratibu huyo alisema kuwa mwitikio kwa wanachi ulikuwa mkubwa kuchangia Damu kwa hiari ili kuweza kuokoa maisha ya watanzania.
Aidha alibainisha kueleza kuwa wamefanikiwa kutimiza lengo huku uhitaji wa Damu katika Hospitali ya Bombo kwa mwezi ikiwa ni uniti 433.
Mratibu huyo,Juma ametumia nafasi hiyo kwa kuwaomba wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kujitokeza kuchangia ili kuwa na akiba ya kutosheleza kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanza hususan wanawake wakati wakujifungua na wale wanaopata ajali ,
Aliongeza kusema kuwa zoezi hilo ni endelevu kufanyika ambapo kwa mwaka jana walifikia kuchangia asilimia 78 ambayo ilikabiziwa hospital ya rufaa Bombo.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji ya WHO IS HUSSEIN FOUNDATION,Azim Dewji alitumia nafasi hiyo kuwataka wadau wengine kujitokeza kuweza kuunga mkono ili kuongeza benk ya damu katika hospital hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment