Pichani ambaye anazungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ni Kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi akithibitisha,CP Awadh Haji nje ya hospital ya Magunga wilayani Korogwe mkoani Tanga akimwakilisha mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP aliwaasa madereva kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali,majeruhi na ulemavu kwa jamii hapa nchini. .
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
AJALI ya magari kugongana uso kwa uso na kusababisha Vifo vya watu 17 huko wilayani Magila Gereza wilayani Korogwe mkoani Tanga imeleta simanzi na majonzi kwa Wananchi huku Serikali ikiwa mstari wa mbele katika kuwafariji wahanga.
Katika ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Coaster iliyokuwa ikisafirisha maiti na Fusso tayari Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefika eneo la tukio.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania,Samia Suluhu Hassan ametoa salaam za pole na maagizo kadhaa kufuatia tukio hilo la ajali ambayo imejeruhi watu wapatao 12 na vifo 21.
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Hemed Suleiman Abdula aliyepo mkoani Tanga, asubuhi alilazimika kukatiza ziara yake na kwenda kuwaona na kuwafariji majeruhi waliolazwa hospitali ya Bombo.
Mganga mfawidhi hospitalini hapo Dkt Naima Yusuph amethibitisha kuwapokea majeruhi huku akitanabaisha kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa Magunga hospitali huko Korogwe.
Akiwa wilayani Pangani Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar aliendelea kuwapa pole wale wote waliofikwa na msiba huo.
Pamoja na Makamu wa Rais huyo naye Kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi CP Awadh Haji amefika mkoani Tanga akimwakilisha mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP.
CP Awadhi aliambatana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kamishna msaidizi,ambapo walipokelewa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga.
Viongozi hao wamefanikiwa kufika eneo la tukio huku kamisha Awadhi akiwaasa madereva kufuata sheria za usalama barabarani na kwamba jeshi halitasita kuchukua hatua stahiki kwa watakaokiuka.
CP Awadh akimwakilisha IGP Camilius Wambura ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa waliokumbwa na kadhia hiyo akiwataka kuwa na subira.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba ambaye ni mwenyekiti ya ulinzi na usalama ameonekana kuwa mstari wa mbele muda wote kushughulikia changamoto hiyo iliyojitokeza.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA.
WAZIRI wa Mambo ya ndani,Hamad Massauni amewataka Wananchi kuendelea kuwa waangalifu na wenye kutii Sheria za Usalama barabarani hatua ambayo itaweza kusaidia kuepuka kuleta madhara kwa Watu wasiokuwa na hatia.
Waziri Massauni ametoa Wito huo jana mara baada ya kuwatembelea na kuwafariji Majeruhi 12 wa ajali iliyohusisha gari aina ya Fuso na Coasta huko katika hospitali ya rufaa Bombo iliyopo Mkoani Tanga.
Katika ziara yake hiyo akizungumza na waandishi wa habari,Waziri Massauni alisema kuwa ni vyema wananchi kuendelea kutii sheria za usalama barabarani ili kuzuia ajali nyingine kutokea.
"Nitoe wito kwa wananchi kuendelea kuwa waangalifu na kutii sheria za usalama barabarani kuepuka kusababisha madhara kwa watu wasio na hatia"alisema.
Akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria,Waziri Massauni alisema, mara nyingi kosa la mtu mmoja linaweza kugharimu maisha ya wengine akitaka kila mmoja kuzingatia sheria.
Waziri huyo wa mambo ya ndani ametumia fursa hiyo kuwapa pole wale waliopatwa na msiba na watanzania wote kwa ujumla wake.
Massauni amesema amekuja Tanga akiwa ametumwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuja kushirikiana pamoja na wananchi katika kipindi hiki kigumu.
Pia amewapongeza madaktari wa hospitali ya Bombo kwa jinsi wanavyoendelea kufanya jitihada za kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali hiyo.
Aidha alisema kwamba,amefurahishwa na mabadiliko chanya yanayoonekana kwenye hospitali ya Bombo katika utoaji huduma kwa wananchi.
Aidha,alisema kuwa maboresho yaliyofanyika kwenye hospitali hiyo katika upatikanaji wa vifaa mbalimbali akitaja vipimo vya Scan imerahisisha upatikanaji wa matibabu kwa haraka.
Massauni alisema, hayo yanayoonekana ni matokeo ya kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira kwenye sekta ya afya.
Pamoja na hayo.,Waziri Massauni hakusita kulipongeza jeshi la polisi kwa ushirikiano mkubwa walioonesha katika tukio la ajali hiyo iliyotoke eneo la Magila Gereza wilayani Korogwe Mkoani Tanga.
Wakati huo huo,Dk. Monica Mmasy ambaye ni Medical Officer idara ya dharura hospitali ya Bombo alisema,wagonjwa waliolazwa wanaendelea vizuri huku akitaja mwanamume mmoja kuhamishiwa Muhimbili na watoto wawili mmoja akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 4 mwingine 6 kuwa wamepoteza maisha.

No comments:
Post a Comment