Pichani ni Afisa mtendaji wa mtaa Kwanjeka A,uliopo kata ya Mnyanjani, Samira Msumari akiwa katika eneo la mradi wa kisima akieleza wamefanikiwa kupata miradi miwili kupitia mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.
NA SOPHIA WAKATI, TANGA.
WAKAZI wa Mtaa wa Kwanjeka 'A' wameelezea kuridhishwa kwao juu ya ujio wa Mradi wa ajira za muda kupitia TASAF wakisema, imewezesha kutatua kero zilizokuwa sugu kwenye maeneo yao.
Hayo yamebainika wakati Mwandishi wa habari hizi alipopata fursa ya kufanya mahojiano na Walengwa wa Mpango wa TASAF kuhudumia Kaya masikini.
Afisa mtendaji huyo wa mtaa wa Kwanjeka A, Samira akiwa katika eneo la mradi huo wa kisima alisema kwamba, mtaa wake wa Kwanjeka 'A' umepata miradi miwili kupitia mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.
Hata hivyo,ameitaja miradi hiyo ambayo imeibuliwa kuwa ni ule wa Uchimbaji wa Kisima cha Maji ambacho kitakuwa mkombozi kuwaondolea wananchi kero ya maji na ule wa Usafishaji mfereji.
Alisema, miradi hiyo inayotekelezwa na Walengwa wa TASAF imewezesha kuleta mabadiko makubwa kwenye mtaa wa Kwanjeka 'A' na kata ya Mnyanjani kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Samira, kabla ya mradi huo wa kisima, nyakati za ukame wananchi walikuwa wanahangaika kusaka maji huduma ya maji na kwamba kwa sasa wanaishukuru serikal kupitia TASAF kuwapatia mradi huo wa ajira za muda.

Miongoni mwa wanufaika,Rehema Athuman Abdallah mkazi wa Kwanjeka A, ametumia nafasi hiyo kuishukuru TASAF kuwawezesha kutatua changamoto ya mifereji kujaa maji na pia kutembea umbali mrefu kusaka huduma ya maji.
Pamoja na mafanikio hayo kupitia ajira za muda, Rehema ameishukuru TASAF kuwawezesha watoto kupata mahitaji ya shule, lishe na hata kuhudhuria kliniki.

Hata hiyo,jumla ya kaya 74 zimefanikiwa kunufaika na mpango wa TASAF katika mtaa wa Kwanjeka A' kata ya Mnyanjani iliyopo halmashauri ya jiji la Tanga.
Mwisho.
Mwisho.
Pichani ni miongoni mwa wanufaika wa TASAF mtaa wa Kwanjeka A,wakitekeleza mradi wa kisima.
No comments:
Post a Comment