UONGOZI wa Kiwanda
cha kuchakata kamba za Mkonge cha Pongwe (Pongwe Spinning Mill) kimeiomba
serikali kuzuia uingizaji wa kamba bandia za nailoni ili kulinda soko la kiwanda
hicho,.
Meneja wa Kiwanda cha Kamba kilicho Pongwe halmashauri ya jiji la Tanga,, Robert Semwaiko ambapo alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba aliyetembelea kiwanda hicho jana kwamba kiwanda kimehujumiwa sana kutokana na kusambaa bidhaa hizo za kamba za nailoni katika masoko.
Kiwanda hicho cha kamba za mkonge cha Pongwe kilicho njie kidogo ya jiji la Tanga kinapata hasara katika uzalishaji kibiashara kutokana na ushindani na bidhaa za kamba za nailoni ambazo huuzwa kwa bei ya chini sana ukilinganisha na bei ya kamba za mkonge,
Semwaiki alisema
awali kiwanda kilikuwa na wafanyakazi wapatao 300, lakini sasa hivi kina
wafanyakazi 160 tu baada ya uongozi kulazimika kupunguza idadi kutokana na
kuanguka soko la bei hiyo.
,Sisi
tunauza kilo moja ya kamba ya mkonge kwa shilingin 5,000/- wakati kamba za
nailoni zinauzwa kwa shilingi 3,000/-.” kwa kilo, Alisema Semwaiko na kuongeza kuwa
huenda kiwanda kitapunguza wafanuyakazi zaidi iwapo kamba hizo bandia
zitaongezeka.
Akizungumza
baada ya kutembelea na kukagua kazi
kiwandani hapo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba alisema ni sera ya serikali
ya kuruhusu biashara huria ili kuleta changamoto , lakini wakati huo huo
kusimamia miongozo ya ufanyaji biashara ikiwa ni pamoja na ulipaji kodi.
Mkuu wa Mkoa
aliahidi kufuatilia suala la kamba
bandia akisisitiza kuwa ufumbuzi utapatikana muda sio mrefu.
“Nia ya
serikali ni kuona wafanyabiashara wanafanya shughuli zao kwa weledi na uaminifu
bila kusahau ulipaji kodi stahiki”, alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment