NA SOPHIA WAKATI, TANGA
MAMLAKA ya bandari ya Tanga,Kwa mara ya kwanza imeweka historia Meli kubwa kutoka Urusi ikiwa na mzigo wa tani 6909.292 za Amonium nitrate imeweza kutia nanga kwenye Bandari ya Tanga.
Meneja wa Bandari ya Tanga,Masoudi Mrisha amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mafanikio ya uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Alisema kwamba Meli kubwa za mizigo zimeanza kutia nanga kwenye Bandari ya Tanga na kufungua fursa kwa wafanyabiashara ili kuweza kuitumia.
Mrisha,kwa kipindi kirefu imekuwa ikifanyiwa maboresho kwa uwekezaji wa Shilingi Bilioni 429.1 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Aidha,alieleza kuwa, mpaka sasa katika maboresho yaliyofanyika wamekabidhiwa Mita 300 na wameweza kupata Meli yenye ukubwa wa Mita 150.
"Mara baada ya kukabidhiwa mita 300,tumepata meli ya ukubwa mita 150 imeleta mzigo wa Amonium nitrate tani 6909.292 inakwenda Congo Lubumbash"alisema meneja huyo wa bandari ya Tanga Mrisha.
Alibainisha kueleza kuwa mzigo huo unatarajiwa kupakuliwa kwa saa 48 na matarajio yao ni kupata meli kubwa zaidi ili kupanua wigo wa biashara kwa wananchi wa mkoa wa Tanga na taifa.
Kuhusu mradi huo maboresho Bandari ya Tanga, Mrisha alisema kwamba umekamilika kwa asilimi 94% ambapo utakabidhiwa rasmi April 4,2023 mwaka huu.
"Mradi umefikia asilimia 94 Aprili 4 tunatarajiwa kukabidhiwa mita zote 450,tutapata meli kubwa zaidi hadi mita 200, tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan matunda yameanza kuonekana"alisema Mrisha.
Mrisha aliongeza kuwa Machi 15 mwaka huu wanatarajia kupakuwa meli ya Petrolium petcok mzigo wa mali ya Sayona na Neelkant ambapo kuna idadi ya tani 51,000.
Pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wadau wakiwemo wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga aliyoieleza kuwa kwa sasa imefunguka na itatoa huduma bora kwa wateja.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha masoko Bandari ya Tanga,Rose Tandiko ametumia nafasi hiyo ,kuwahamasisha wadau kuitumia bandari ya Tanga kwa maelezo kuwa imekamilika na wako tayari kwa ajili ya kuwahudumia.
Amesema kuwa Mamlaka ya bandari ya Tanga inamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika bandari hiyo ambao matokeo yake yameanza kuonekana.
Mwisho.

Pichani ni Meli kubwa kutoka Urusi ikiwa na mzigo wa tani 6909.292 za Amonium nitrate ikiwa imetia nanga kwenye Bandari ya Tanga.
No comments:
Post a Comment