Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa Magila Falls Eco Resort.Dkt. David Mchaina akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mara baada ya kutembelea vivutio vilivyopo magila falls
NA SOPHIA WAKATI,MUHEZA
Mkurugenzi mtendaji wa Magila Falls Eco Resort.Dkt. David Mchaina aliyasema hayo katika Mahojiano na mwandishi wa makala hii wilayani Muheza Mkoani Tanga.
Dkt Mchaina alisema kuwa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya kitu cha kipekee kwa kufanya Royal Tour ambayo imesaidia kukuza utalii utakaokuza mapato ya nchi.
Dkt Mchaina ambaye ni Mwekezaji mzawa kwenye sekta ya utalii kupitia kampuni yake ya Magila Falls Eco Resort alishauri umimarishwaji wa suala kuwahudumia wageni wanaokuja kutembelea maeneo ya utalii nchini Tanzania.
"Rais kuanzisha Royal Tour amefanya kitu special, imesaidia kuongeza ari ya utalii nchini Tanzania" alisema Dkt Mchaina.
Dkt Mchaina alieleza kwamba, utalii wa ndani unakua kwa kasi nchini ambapo kwenye uwekezaji wake ameshuhudia idadi kubwa ya vijana chini ya miaka 35 wakitembelea Magila Falls Eco Resort.
Kwa upande mwingine Dkt Mchaina alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kujikita katika suala la utunzaji mazingira.
Aidha alibainisha kueleza kwamba,katika uwekezaji amekuwa akizingatia utunzaji mazingira yakiwemo yale ya vijito jambo ambalo limesaidia kuleta manufaa makubwa kwa jamii nzima.
Aliongeza kusema kuwa, elimu ya uhifadhi inapaswa kuendelea kutolewa kwa umma na kila mmoja anapaswa kutambua kuwa anawajibika kulinda rasilimali asilia ambazo ni tunu kwa Taifa.
Pamoja na hayo amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi za serikali katika mikakati yake ya kuihamsisha jamii umuhimu wa Utunzaji mazingira.
Mwisho.

ReplyForward |
Eneo la mahema kwa ajili ya kulala wageni wanaotembelea katika eneo la magila Falls
Pichani ni waandishi wakitembelea vivutio magila Falls
Waandishi wakipata maelekezo kutoka kwa waongoza wageni Magila Falls.
Picha ni eneo la mapokezi magila Falls.
No comments:
Post a Comment