NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KAMPUNI ya Turkana inayosimamia kitengo cha upakiaji na upakuaji katika kiwanda cha Huaxin kilichoko kata ya Maweni Halmasauri ya Jiji la Tanga ina mpango mkakati wa kuboresha mazingira ya maslahi ya wafanyakazi ili kuweza kuleta tija kazini.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Turkana General Enterprises, Michael James wakati akizungumza na wafanyakazi kiwandani hapo ambao waligoma kufanya kazi kutokana kukabiliwa na changamoto mbalimbali kugoma ikiwemo kulalamikia mishahara duni na isiyolingana na makubaliano.
Michael alikiri na kueleza kwamba madai yote ya wafanyakazi hao wa kitengo cha upakiaji na upakuaji ameyachiukua na atakayaanyia kazi kwa ahadi kuwa atayaboresha ikia ni ni pamoja na kutoa mikataba kwa wale wenye ujuzi na uzoefu wa kazi hizo.
Hata hiyo, ahadi hiyo imekuja mara baada ya wafanyakazi wapatao 70 kufanya mgomo wa siku moja ambapo ulisababisha athari nyingi ikiwemo msongamano usio wa kawaida wa magari uliofika hadi kwenye foleni ya kupakia mizigo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo alilazimika kuendesha mkutano wa dharura na wafanyakazi lengo ilikiwa ni kurudisha amani iliyopo na kuleta mshikamano baina ya uongozi wa kampuni hiyo na wafanyakazi.
Alifafanua kwamba katika kampuni hiyo ya Turkana, inayosiamamia kitengo cha upakiaji na upakuaji ina jumla vijana wapatao 70 wakiwemo wanaochukua uzoefu wa kazi ambao watapangiwa utaratibu mzuri ili waweze kunufaika na fursa zilizopo na kujiongezea kipato.
Awali wafanyakazi hao wa sekta ya upakiaji mizigo walifanya mgomo wa siku moja wakilalamikia kutoridhishwa na malipo hafifu pamoja na kutokuwa na mikataba ya kazi na kutowekewa akiba zao katika hifadhi za jamii kama vile NSSF ili kuwezeshwa kunufaika na mafao yao ya uzeeni.
“Nilipigiwa simu na uongozi wa kiwanda na baadhi ya wafanyakazi nikiwa safarini kunifahamisha kuhusu mgomo huo wakilalamikia kutotendewa haki katika masuala ya ajira, mishahara na malupulupu mengine”, alisema Micheal.
Mkurugenzi huyo alibainisha adhma yake ya kutimiza madai ya wafanyakazi hao ili kuleta tija na kuwataka kuendelela kuwaamini viongozi wao katika kutatua changamoto zinazowakabii sehemu za kazi.
Nae,Meneja wa NSSF mkoani Tanga,Audrey Laudyus akizungumza na wafanyakazi kiwandani hapo amesema analichukua suala hilo kufanya uhakiki lengo kubaini wanawekewa mafao.
Kwa upande wake Afisa kazi mkoa wa Tanga,Janeth Omolo amesema ataketi na uongozi wa kiwanda hicho kuondoa changamoto zilizopo na kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa mishahara yao kwa wakati.
Mwisho.
Miongoni mwa wafanyakazi wakiendesha mgomo kiwanda cha Huaxin.
No comments:
Post a Comment