Sunday, 5 March 2023

KAMPUNI YA ORYX GAS TANZANIA YA GAWA MAJIKO 800 KWA WAJASILIAMALI WA JIJI LA TANGA,,,,,,

Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa akiwaeleza wajasiliamali kwamba kitendo kilichofanywa na Mbunge wa jimbo la Tanga, kitaacha alama kwa kada ya wanawake kwenda kutimiza malengo yao na sehemu ya kuondoa changamoto kwenye jamii ya ukataji wa miti inayopelekea kuharibu mazingira.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KAMPUNI isiyo ya kiserikal ya Oryx Gas Tanzania imetumia zaidi ya million 30 kwa ajili ya kukabidhi mitungi ya gesi wanawake wasiriamali ili kuwawezesha kutumia muda mchache jikoni.

Mbunge wa Jimbo la Tanga ambaye pia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu  katika uzinduzi huo wa kukabizi majiko hayo uliofanyika jijini Tanga alisema matumizi ya nishati ya gesi itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira.

Alisema kuwa majiko hayo yametolewa kwa wanawake 600 kutoka vikundi mbalimbali vikiwemo vya wajasiriamali katika Mkoa wa Tanga ili kurahisisha majukumu yao.

Alisema kuwa lengo ni mkakati wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na wanawake kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa yanayoharibu mazingira hapa nchini.

 Aidha,alitumia nafasi hiyo kuishukuru Kampuni hiyo ya Oryxs Gas Tanzania kwa kuridhia ombi lake la kukubali kuwasaidia wanawake wajasiriamali kutoka vikundi vilivyopo kwenye Kata zote za Jimbo la Tanga.
  
''Wanawake wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali ambao mmefanikiwa kunufaika na kampuni hii,mkawe mabalozi kwenye maeneo yenu,kuwahamasisha wanawake kutumia nishani ya gesi kuokoa muda jikono'alisema Waziri Ummy.

Nae Mkurugenzi wa ORYX GAS Tanzania,Araman Benoite alisema kwamba kutokana na madhara yanayotokana na mkaa kuni duniani, imegushwa na kurudisha fadhila zake kwa wanawake wajasiriamali mkoani Tanga.

Alisema kampuni hiyo iko mstari wa mbele kusaidia lengo likiwa kuunga mkono jitihada za serika kuhamasisha matumizi ya gesi safi ya kupikia kwa kutoa mchango mwingine wa vifaa vya majiko mkoani Tanga ambako matumizi ya mkaa ni makubwa.

''Matumizi ya mkaa yana athari kubwa kwa mazingira yetu, husababisha jangwa na Tanga ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo ina idadi ya juu ya ukataji miti kwa ajili ya mkaa''Alisema.

Mkurugenzi huyo wa ORYX GAS Tanzania,Araman,alisema kwamba wao wanaamini mpango huo wa kusaidia vifaa kwa wajasirimali utasaidia wakazi wa jiji la Tanga, hasa wale ambao wanaathirika na moshi unaotokana na kuni au mkaa  kutimiza majukumu yao ya jikoni kwa tija.

"Kiukweli kampuni itawawezesha kwa kutekeleza miradi ya kutoa elimu juu ya gesi safi ya kupikia, inachangia vifaa vya gesi ya kupikia katika baadhi ya mikoa.Pia tunahamasisha matumizi ya gesi kwa kufanya mauzo makubwa ya mitungi kwa bei nafuu.

Aidha,alisema kuwa Juhudi zote hizi zinalenga kufanya Watanzania wengi wanaanza kutumia gesi safi ya kupikia kama alivyoahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan.

''Ndugu zangu Rais Samia Suluhu Hassan ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia gesi safi ya kupikia''alisema Mkurugenzi huyo wa ORYX GAS Tanzania,Araman.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa alisema kitendo kilichofanywa na Mbunge huyo kitaacha alama kwa kada ya wanawake kwenda kutimiza malengo yao na sehemu ya kuondoa changamoto kwenye jamii ya ukataji wa miti inayopelekea kuharibu mazingira.

“Matumizi ya gesi nchini bado yanakwenda kwa kusuasua kwa hiyo kupitia hili kutakuwa na ushawishi mkubwa kwa kuhakikisha jamii inatumia nishati mbadala ya gesi ambayo itasaidia kutunza mazingira na kuondoa uharibifu wa mazingira” Alisema

Awali, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Al- Shaymaa Kweygir alisema kwamba wanashukuru Mbunge Ummy Mwalimu kwa kuwajali wakina mama kwa sababu wao wana mchango mkubwa kwa maendeleo .

Alisema kwamba kitendo cha kuwezeshwa majiko ya Gesi kwa wajasiriamali wanawake itawasaidia kuwakomboa kichumi kwa sababu wanapokuwa kwenye shughuli zao watakuwa wakitumia muda mchache kuandaa na kuwahuduma wateja wao.

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Abdurhaman Shiloo alimshukuru Mbunge Ummy kwa kuendelea kuwajali wananchi na Baraza la Madiwani linamshukuru kwa kuhakikisha maendeleo kwenye Jimbo hilo yanaendelea kupaa.

Hata hivyo,alisema kwamba Mbunge huyo niwa kipekee na haijawahi kutokea kwa Jimbo hilo tangu lilipoanzishwa ameacha alama na kuvunja rekodi ya wabunge wengine waliowahi kuliongoza Jimbo hilo .
Mwisho


Pichani ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Abdurahman Shiloo akiMwalim mshukuru Mbunge Ummy kwa kuendelea kuwajali wananchi ikiwemo wajasiriamali.



Pichani ni Mkurugenzi wa ORYX GAS Tanzania,Araman,akikabizi majiko kwa ajili ya kusaidia wajasirimali wa jiji la Tanga, hasa wale ambao wanaathirika


Pichani ni Mkurugenzi wa ORYX GAS Tanzania,Araman,akieleza lengo na mpango wake wa kusaidia vifaa kwa wajasirimali utasaidia wakazi wa jiji la Tanga, hasa wale ambao wanaathirika na moshi unaotokana na kuni au mkaa  kutimiza majukumu yao ya jikoni kwa tija.

No comments:

Post a Comment