Wednesday, 8 March 2023

RUWASA MKOANI TANGA,JINSI ILIVYOJIPANGA KUPELEKA HUDUMA YA MAJI YAKUTOSHELEZA KWA WANANCHI WA MSOMELA,,,

Pichani ni Meneja wa RUWASA Mkoani Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo akieleza mpango mkakati uliopo kuhakikisha wananchi wa Msomela wanapata maji ya kutosheleza hitaji.

NA SOPHIA WAKATI,HANDENI
WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Mkoani Tanga wamesema,mahitaji ya Maji katika Kijiji cha Msomera yameongezeka kufikia Mita za ujazo 450 kwa siku kwa kuzingatia matumizi ya wastani wa lita 25 kwa mtu mmoja kwa siku pamoja na mahitaji ya huduma hiyo kwenye taasisi.

Meneja wa RUWASA Mkoani Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo alitoa taarifa hiyo juzi ambapo alisema kwamba kufuatia ujio wa wananchi waliokubali kuhamia kijiji cha Msomera wilayani Handeni kwa hiari kutoka Ngorongoro idadi ya wakazi inatarajiwa kuongezeka kutoka 7,967 hadi kufikia 17,000.

Kutokana na hali hiyo Mhandisi Pendo alisema,ili kuhakikisha wakazi waishio Msomera na wakazi wapya wa kijiji hicho wanapata Maji safi na salama toshelevu, serikali kupitia RUWASA imefanya utafiti wa vyanzo vya maji vya uhakika.

AAidha,alisema kuwa Vyanzo hivyo ni vile vitakavyowezesha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kiasi kisichopungua mita za ujazo 450 kwa siku.

Kwa mujibu wa Mhandisi huyo wa maji ambaye ni Meneja wa RUWASA Mkoani Tanga,alisema vyanzo vilionekana kuleta matumaini vitaleta matokeo mazuri ni vyanzo vya maji juu ya ardhi kupitia ujenzi wa bwawa na vyanzo vya maji chini kupitia uchimbaji visima virefu.

Aidh,alisema kazi ya uchimbaji wa visima virefu ilianza kwa tafiti ambapo bodi ya bonde la mto Pangani na Kampuni ya Wema Consult Limited zilifanya tafiti ya maji chini ya ardhi na kisha kazi ya uchimbaji kuanza.

Mhandisi Pendo alisema kwamba visima 18 tayari vilichimbwa ambapo kati ya hivyo visima vitano vilipata maji yanayofaa kwa matumizi ya binadamu.

Alisema kwamba visima vilivyochimbwa vina uwezo wa kuzalisha maji mita za ujazo kwa saa 2,5,3,7,8 na 19.8 hivyo kuwezesha upatikanaji maji jumla ya mita za ujazo 775.2 kwa siku.

Kuhusu ujenzi wa bwawa,Mhandisi Pendo alisema, Serikali kupitia wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA imeingia mkataba namba AE-102/2021-2022/TAG/W/72 na Kampuni ya Chelesi General Enterprises LTD.

Mkataba huo ni ule wa ujenzi bwawa hilo la maji unaogharimu Tsh 1.99 bilioni utekelezaji wake ukiwa kipindi cha miezi 12 ingawa matarajio ni kazi kukamilika kabla ya muda uliopungwa.
mwisho.

Pichani ni Meneja wa RUWASA Mkoani Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo akisoma taarifa yake kwa waandishi wa habari, kufuatia ujio wa wananchi waliokubali kuhamia kijiji cha Msomera wilayani Handeni kwa hiari kutoka Ngorongoro idadi ya wakazi inatarajiwa kuongezeka kutoka 7,967 hadi kufikia 17,000.


 Pichani ni miongoni mwa wakandarasi wakiwa katika ukumbe wa halmashauri ya jiji la Tanga zoezi la kusaini mikataba ya utekelezaji miradi ya maji mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment