Picha Mkono wa kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Kamishna William Mwakilema akipokea Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Handeni,Jafari Becha kushoto hafla iliyofanyika shule ya wasichana Korogwe Girls iliyopo wilayani hapo.
NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
MIRADI sita ya maendeleo ya wananchi iliyogharimu zaidi ya shilingi za kitanzania Billion moja,imekaguliwa,kufunguliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga.
Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Ismail Ally Usi,Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Kamishna William Mwakilema alisema katika miradi sita ipo itakayotembelewa,kuwekewa jiwe la msingi na kukaguliwa.
Awali Mkimbiza Mwenge Kitaifa,Ismail Ally Usi aliwataka wataalaam na watendaji kuhakikisha taarifa zote muhimu za miradi hiyo itakayotembelewa na Mwenge kuhakikisha zinakuwepo maeneo ya miradi sambamba na wataalam wahusika.
Kuhusu Mwenge wa Uhuru,Ismail alisema rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julias Nyerere aliamua upandishwe mlimani Kilimanjaro kwa lengo la kumulika ukiangaza maeneo ya nchi ikiwa kiashiria cha kuimarisha Amani na kuleta na kuleta matumaini kwa Umma.
Alisema kwamba Halmashauri ya Mji Korogwe imetoa shilingi million 40 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wa kikundi cha Bajaji na bodaboda ili kuweza kuimarisha shughuli zao za usafirishaji wilayani hapo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mmoja wa wanakikundi hao,akimweleza Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,Ismail kuwa halimashauri yao imewawezesha ili kuweza kuboresha biashara yao ya usafirishaji na hivyo kuimarisha uchumi wao.
Msoma taarifa huyo alisema awali walianzisha kikundi chao hicho wakiwa na mtaji wa shilingi million 14 kabla ya serikal kupitia halmashauri kwa kutumia mapato ya ndani kuwapatia million 40hapo January 2022.
Alisema kuwa,baada ya kuwezeshwa fedha hizo na halmashauri waliongeza mtaji wao kwa kununua bajaji tatu huku wakiimarisha duka lao la vilainishi hatua ambayo imesaidia kukuza mtaji wao.
Akibainisha kuwa hivi sasa mtaji wao umekuwa na kuongezeka hadi kufikia shilingi million 54 za kitanzani huku wakifanikiwa kufanya marejesho kwa zaidi ya shilingi million sita.
Aidha,kupitia uimarishaji biashara yao hiyo vijana hao wa bodaboda na bajaji mbali na kujiajili kwa manufaa lakini pia wameweza kuajiri vijana wenzao ambao ni mafundi pikipiki.
Wameishukuru serikal kwa kuwapatia fedha hizo za mikopo ya asilimia kumi wakisema zimewasaidia kuongeza mtaji na kubadilisha maisha yao.
Mwisho.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Ismail mara baada ya kuwasili wilayani Korogwe akiwasalimia viongozi na watumishi mbalimbali wilayani hapo.
No comments:
Post a Comment