NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KLABU ya Coastal Union yenye maskani yake Jijini Tanga, imezika tofauti walizokuwa nazo awali zilizosababisha timu hiyo ishuke kutoka Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2014/ 2015, na sasa timu hiyo imeunda umoja wa viongozi utakaokuwa na lengo la kuirejesha Ligi Kuu msimu ujao.
KLABU ya Coastal Union yenye maskani yake Jijini Tanga, imezika tofauti walizokuwa nazo awali zilizosababisha timu hiyo ishuke kutoka Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2014/ 2015, na sasa timu hiyo imeunda umoja wa viongozi utakaokuwa na lengo la kuirejesha Ligi Kuu msimu ujao.
Akizungumza LEO saa tano asubuhi kwenye mkutano wa wanachama
uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo barabara ya 11 Jijini hapa,
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano, Ahmed Hilal maarufu ‘Aurora’ alisema
kutokana na kikao kilichofanyika katika hoteli ya Mkonge, kimezika
tofauti hizo na sasa wapo pamoja.
Alisema miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano huo
uliorudisha umoja ni pamojana,Nassor Binslum ambaye ataisaidia tena
klabu hiyo pamoja na watu wengine ili kuhakikisha timu hiyo
itakayoshiriki Ligi Daraja la kwanza iweze kurejea Ligi
Kuu.
“Kiukweli mkutano uliofanyika Mkonge
Hoteli umezika tofauti zote ambazo zilijitokeza awali na tumeunda umoja
ambao umewezesha timu yetu kusajili
wachezaji watakaokuwa na uwezo wa kupanda daraja,Tunachotaka sasa watu
wote wajali Coastal kwanza mambo mengine ya baadaye,”
alisema Aurora.
Hata hivyo,Coastal iliteremka daraja baada ya viongozi kuhitafiliana na
Aurora akiwa Mwenyekiti aliyeipandisha daraja timu hiyo
msimu wa 2011-2012 alijiuzulu wadhifa huo na baadaye timu kufanya
uchaguzi uliomweka madarakani Dk. Ahmed Twaha ambaye aliishusha daraja
akiwa na katibu wake Kassim
El-Siagi na Akida Machai.
Mgogoro huo ulisababisha baadhi ya watu kwenda
kujiunga na timu ya Mgambo JKT ambayo nayo ilishuka daraja hadi la
kwanza huku wanachama wengine wakienda katika timu hiyo ambapo zote
mwaka jana ziliposhiriki ligi daraja la kwanza hazikufanya
vizuri.
“Tumesameheana kabisa na sasa tupo pamoja, tusianze
kunyoosheana vidole na kufukua makaburi yaliyipita hatutafika
tunapotaka kwenda lakini lazima mkumbuke mpira sasa ni
fedha…Nawakumbusha pia lipeni ada zenu muwe na sauti kwa viongozi hawa,”
alisema Aurora.
Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo,Mohamed Musni,
alisema kwamba hivi sasa uongozi wa klabu hiyo umepanga kuhakikisha
inafanya vizuri katika Ligi daraja la kwanza itakayoanza mwezi ujao ili
waweze kurejea kwa kishindo Ligi Kuu.
Nae Mjumbe wa kamati ya utendaji ya timu hiyo Abdallah
Zuberi ‘Unenge’, aliwataka wanachama kuhakikisha wanaacha majungu ya
kupeleka habari zitakazowarudisha kule walipotoka na badala yake
wahubiri umoja kwa faida ya timu hiyo.
Kwa upande wake kaimu Katibu Mkuu,Nassoro Kibabedi, alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka
wanachama waisaidie timu hiyo katika kipindi hiki na kamwe wasibweteke
wakiamini kwamba wafadhili watafanya kila kitu hivyo walipeada zao ili
ziweze kuisaidia klabu hiyo.
Mwisho.
Mwisho.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TIMU ya soka ya Coasta Union ya Jijini hapa, itaanza mazoezi kesho (Jumanne) kwenye uwanja wa Mkwakwani kujiwinda na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), inayotarajiwa kuanza mwezi ujao huku ikitangaza nyota wake wapya iliyowasajili msimu huu.
TIMU ya soka ya Coasta Union ya Jijini hapa, itaanza mazoezi kesho (Jumanne) kwenye uwanja wa Mkwakwani kujiwinda na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), inayotarajiwa kuanza mwezi ujao huku ikitangaza nyota wake wapya iliyowasajili msimu huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo,Ahmed
Hilal maarufu ‘Aurora’, alisema kazi ya usajili haina rahisi kutokana na kwamba
kabla hawakuwa na fedha hivyo baada ya kurudisha umoja wameweza kusajili
wachezaji wadhoefu watakaowasaidia kupanda
daraja msimu huu.
Aurora aliwataja baadhi ya wachezaji wapya kuwa ni
pamoja na mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taiufa Stars’, Simba na
Yanga Athumani Idd ‘Chuji’, Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Salvatory Ntebe
kutoka Ndanda FC, Ramadhani Hassain kutoka
Mbeya City, Maulid Rajab ‘Mau’ African Sports, Hilal Juma Mtibwa,
Ramadhani Mussa Pamba, Ibrahim Ndanda, Baraka Jafar na Omary Salum
kutoka African Lyion.
Huku wachezaji wengine ni
pamoja na mfungaji bora wa Ndondo Cup iliyomalizika hivi karibuni Jijini
Dar es salaam Rashid Roshi, Exavery Emanuel, Rahim Aziz Afrikan Lyion,
Sagaf
Kabaki, Bakari Mtwiku, Bakari Nondo, Said Jeilani na Abubakari Kinanda ‘Mapara’ kutoka malindi ya Zanzibar.
Katibu wa klabu hiyo,Nassor Kibabedi alisema
mazoezi yataanza kesho kwenye uwanja wa Mkwakwani asubuhi kishajioni
yatafanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Galanos ambako mwalimu
atakuwa Joseph Lazaro.
Mwisho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment