Pichani ni Mhifadhi mkuu wa
Nilo,Fabian Mukome juzi akizungumzia lengo la kuandaa Washa hiyo ni kuwakutanisha Wadau
wa sekta ya utalii ili kuwapatia uelewa juu ya vivutio vya utalii vinavyo
patikana kwenye hifadhi hiyo ya Nilo iliyopo Wilayani Korogwe mkoani Tanga.
WADAU wa sekta ya Utalii wametakiwa
kuhakikisha kuwa wanakuwa mabalozi wazuri wa mhifadhi mkuu wa
Nilo,Fabian Mukome amesema lengo la kuandaa Washa hiyo ni kuwakutanisha Wadau
wa sekta ya utalii ili kuwapatia uelewa juu ya vivutio vya utalii vinavyo
patikana kwenye hifadhi hiyo ya Nilo iliyopo Wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Afisa wa Maliasili Mkoani Tanga,
Timothio Sosiya ametoa rai hiyo juzi wakati akifunga washa ya siku mbili ya
wadau yenye lengo la kuwajengea uelewewa juu ya vivutio vya utalii ndani ya
hifadhi ya Mazingira ya Nilo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi veta
Jijini Tanga.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na wadau
mbalimbali kutoka mikoa ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga ambapo alisema kuwa
waongozaji watalii,wamiliki wa Hoteli na chama cha Waandishi wa Habari za
mazingira TARUJA wanayo nafasi kumbwa ya kutangaza vivutio vinavyopatikana
katika hifadhi hiyo.
"Wakati umefika sasa kwa wadau
kila mmoja wetu kuchukua nafasi yake kutangaza vivutio vya utalii kwenye maeneo
yetu,aidha hii hifadhi ya Nilo tusaidiane kuitangaza"alisema Ofisa huyo wa
maliasili mkoani hapo Sosiya.
Kwa upande wake mhifadhi mkuu wa
Nilo,Fabian Mukome amesema lengo la kuandaa Washa hiyo ni kuwakutanisha Wadau
wa sekta ya utalii ili kuwapatia uelewa juu ya vivutio vya utalii vinavyo
patikana kwenye hifadhi hiyo ya Nilo iliyopo Wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Miongoni mwa wadau walioshiriki
Warsha hiyo,Nelvine Peter kutoka Gladys Safari mkoani Moshi amepongeza jitihada
zilizoanzishwa kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa kuitangaza vivutio vya
utalii kwenye maeneo yao kuleta tija kwa jamii mzima.
Agnes Mkala kutoka Panama Gaden
hotel mkoani Moshi alisema kuwa kupitia Warsha kama hizo zimeweza kuwasaidia
kubainika mambo mengi ambayo awali wakikosa kuyafahamu ambapo sasa watachukua
hatua kuvitangaza vivutio vilivyopo.
Aidha Wadau hao wakati wa
kuhitimisha Washa yao wametembelea kwenye hifadhi hiyo ya Nilo iliyopo wilayani
Korogwe ili kuangalia vivutio mbalimbali ikiwemo maua na Vinyonga wenye mapembe
ambao wanapatikana kwenye hifadhi hayo pekee hatua itakayosaidia kuutangaza
utalii na kukuza uchumi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment