Wednesday, 23 November 2022

UCHAGUZI MKUU WA CCM MKOA WA TANGA 2022,,,,RAJABU ANG'ARA,,AVAA VIATU VYA SHEKIFU,,


Pichani ni Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga,Rajabu Abdulrahman mara baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo akiwahutubia wanachama kuweka wazi vipaumbele vyake katika utekelezaji Ilan kuelekea Uchaguzi wa 2025.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

CHAMA Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga, kimepata mwenyekiti mpya na kufanikiwa kukamilisha safu yake ya Uongozi baada ya Rajabu Abdulrahman kuchaguliwai nafasi Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama hicho tawala.

Abdulrhaman katika awamu iliyopita alipata kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani iliyopo Mkoani Tanga.

Katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa Legal Naivera, Abdulrahman alishinda wadhfa huo baada ya kufanikiwa kupata kura 1,340.

WanaCCM wengine waliowania nafasi hiyo mbali na Abdulrahman ni Mathias Mkingwa kura 29 na Dereki William kura 9 ambapo jumla ya kura zote zilizopigwa zilikuwa 1,384 kura halali 1,378 na zilizoharibika 6.

Uchaguzi huo Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga,Pia umefanyika ambapo Mohamed Said maarufu RATCO amefanikiwa kutetea wadhfa huo wa UNEC.

Mohamed Said RATCO ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 774.huku akiwabwaga makada wenzake wawili.

RATCO katika kinyang'anyiro hicho alikuwepo na Omari Sempoli aliyepata kura 563 na Hassan Bomboka kwa kura 45.

Pia katika uchaguzi huo walichaguliwa wajumbe wawili kupitia wilaya ya Tanga ambao ni Habiba Namalecha aliyepata kura 507 na Nassar Makau kura 493.
Mwisho.


 Pichani ni Msimamizi wa uchaguzi huo,John Mongella akimtangaza,Kada Rajabu Abdulrahman mara baada ya kuchaguliwai nafasi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kwa kupigiwa kura 1340,uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa Legal Naivera jijini Tanga.


Pichani ni miongoni mwa wajumbe,Waziri January Makamba akiwa kwenye mchakato wa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa CCM mkoa wa Tanga.  






No comments:

Post a Comment