Thursday, 9 February 2023

MBOWE AFUNGUKA TUTATUMIA VYEMA MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA KUJENGA DEMOKRASIA KATIKA TAIFA,,,

Pichani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, akieleza lengo la ziara yake ya siku mbili jijini Tanga na ataitumia vyema kujenga Demokrasia katika Taifa.

 NA SOPHIA WAKATITANGA

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema kwamba baada ya kuruhusiwa kufanyika kwa mikutano ya vyama vya Siasa, wao wameanza kuitumia nafasi hiyo vyema kujenga Demokrasia katika Taifa.

Ameyasema hayo jana katika mahojiano yake na waandishi wa habari yaliyofanyika Tanga jijini Tanga muda mfupi baada ya kufika ya kuwasili.


"Zuio lile limeondolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tunampongeza na jambo hilo ni jema kwetu.Na sisi tunatumia nafasi hiyo ipasavyo kuijenga Demokrasia katika Taifa"alisema Mbowe.

Mbowe amesema, amewasili kwa ziara yake ya siku mbili ya kikazi kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama chao na kushirikiana na uongozi wa Mkoa huo wa Tanga ili kuweza kuketi.

Amesema kuwa, lengo ni kujua mipango ya uongozi wao katika eneo hilo la nchi hasa uimarishaji chama,kujipanga na chaguzi ndani ya chama na kukipeleka chama kwenye chaguzi zijazo.

"Nimekuja sina ziara nitakuwa na mikutano ya ndani siyo ya hadhara, nitaketi na viongozi mkoa wa Tanga, wa kamati za uongozi kwa maana ya kamati tendaji kisha tutapanga mambo mbalimbali"alisema.

Aidha,Mbowe amesema kuwa ziara hiyo ya siku mbili mkoani hapo amesema lengo la kikao hicho pia ni kuandaa wagombea katika majimbo yote ya mkoa wa Tanga.

Ameelezea mikakati hiyo kuwa sehemu ya kujiimarisha baada ya kufungiwa kufanya siasa kwa zaidi ya miaka saba kipindi alichosema kwamba kiliwaathiri na kuwaumiza.

Aidha,pia ameelezea kuridhishwa kwake kurejeshwa kwa mikutano ya hadhara hapa nchini kama Katiba na Sheria zinavyoruhusu.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment