Friday, 17 February 2023

WANANCHI ELFU 5200 WA KWAKAEZA A WANATARAJIWA KUONDOKA NA MAFURIKO KUPITIA MPANGO WA TASAF,,,

Pichani ni Mwenyekiti wa mtaa Kwakaeza A' ,Abubakari Ally akiwa eneo mradi wa mfereji ambalo limenufaika kupitia TASAF Mradi wa ajira za muda akielezea jinsi ulivyopokelewa na wananchi wa eneo hilo. .

NA SOPHIA WAKATI, TANGA
wananchi wa Kwakaeza A,iliyopo kata ya Mabawa halmashauri ya jiji la Tanga,wamesema mradi wa kusafisha mfereji mama ulioibuliwa na TASAF utasaidia kuwaondolea kero ya muda mrefy ya kukumbwa na mafuriko katika nyumba zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tasaf mtaa wa Kwakaeza A' ,RICHARD Charamila eneo ambalo pia limenufaika kupitia Mradi wa ajira za muda.

Charamila amesema kwamba, kwenye eneo lao la mtaa wa Kwakaeza 'A' ambao wamefanikuwa kuwa na walengwa 37  na amasa katika utekelezaji wa mradi huo.

Pia amesema kupitia mpango huo wa TASAF wamepata manufaa makubwa kuboresha maisha yao ikiwemo kuongeza uchumi na kusomesha watoto.

Chalamila akizungumzia zaidi mradi mafanikio ya mradi huo utakuwa mkombozi kero ya mafuriko maji kuingia ndani ya nyumba zao kipindi cha mvua.

Pia ametumia nafasi hiyo kupongeza juhudi za Serikali kupitia TASAF na uongozi wa kata yao kuwezesha Wakazi wake kuwa miongoni mwa walengwa mradi wa ajira za muda.

Amebainisha kueleza kwamba, wao wameanza utekelezaji mradi huo februari 7, 2023 na kwamba kazi zinakwenda vizuri kwa ushirikiano lengo kukamilika kwa wakati.

"Kiukweli mradi huu niwa siku 60 utekelezaji wake na nguvu kazi ushirikiano ni mzuri watu wamehamasika utakamili kwa wakati"alisema Charamila.

Charamila ameipongeza Serikali kwa jitihada zake huku akiwakumbusha wananchi umuhimu wa kuiunga mkono Serikali yao.

"Tumsaidie Rais kwa vitendo, nchi itajengwa na wananchi wenyewe, tuko tayari kupokea mradi au jambo lolote jipya tutakaloletewa"alisema Charamila.

Kwa upandf wake Mwenyekiti wa Kwakaeza A,Abubakari  Ally amesema eneo hilo limebeba kero kubwa ya mafuriko maji hayaendi kwenye mfereji mkubwa ambapo mvua ya dakika tano huibua mafuriko kwa wakazi elfu 5200 watanusurika.

Amesema kuwa mtaa huo uko bondeni maji yanayotoka kwenye jiji la Tanga yanaingia kwenye kaya na kusababisha mafuriko lakini kukamilika kwa mradi huo utaondoa changamoto hiyo.
Mwisho.


Pichani ni Mwenyekiti wa mradi wa TASAF mtaa wa Kwakaeza A' ,Richard Charamila amesema mradi unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati.






 Picha ni miongoni mwa wananchi wa Kwakaeza iliyopo kata ya Mabawa halmashauri ya jiji la Tanga,wamesema mradi wa kusafisha mfereji mama ulioibuliwa na TASAF utasaidia kuwaondolea kero ya muda mrefy ya kukumbwa na mafuriko katika nyumba zao.


No comments:

Post a Comment