Sunday, 5 March 2023

CHUMA CHAKAVU IMETAMBA KUWA WABABE KATIKA MICHEZO YAKE ITAKAYO SHUKA DIMBANI NA TIMU YOYOTE NCHINI.............


Pichani ni kikosi cha timu ya veterani chuma chakavu yenye masikane yake jijini tanga kikiwa katika uwanja mpya wa TANGA PARK uliopo maeneo ya Raskaoni.

NA SOPHIA WAKATI TANGA.
Timu ya soka ya veterani Chuma Chakavu ya jijini tanga imetamba kuhakikisha iafanya vizuri katika michezo yake mbali mbali itakayoshuka dimbani na club yeyote ambayo iajitokeza kushindana nayo

Matambo hayo yametolewa jana na miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo na Ramadhani Msangawizi maarufu (mbrazil)  katika uwanja wa Usagara secondari.

Mchezaji huyo Mbrazili alisema mara baada ya kucheza mchezo wa fainali wa bonanza lililo andaliwa na bongo muvi ambapo walitoka kwa matokeo ya 5 -4 kwa mikwaju ya penati.

Hata hivyo amesema katika bonanza hilo walifanikiwa kucheza michezo miwili ambapo awali walishuka dimbani na mandingo Veterani kwa kuifunga goli moja kwa nunge nakupelekea mandingo kuyaaga mashindano hayo na Chuma Chakavu kupata nafasi ya kutinga fainali hizo.

Pia miongoni mwa michezo ambayo wameweza kushiriki na kufanya vizuri ni bonanza la ufunguzi wa uwanja mpya wa Tanga Park ambalo lilishirikisha tim 6 na  Chuma Chakavu kuibuka na ubingwa.

Mwisho.




 

No comments:

Post a Comment