Pichani ni Meneja masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanga,Dalton Mgina amesema ufadhili huo unakuja kupitia mchezo wa Ready.
Na Sophia Wakati, Tanga
KUPITIA mchezo wa Ready Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Mkoani Tanga imeanza kurejesha faida wanayopata katika kusaidia huduma za kijamii.
Hatua hiyo ni sehemu ya mchango wa Vodacom kutokana na faida wanazopata kupitia bidhaa zake.
Meneja masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanga,Dalton Mgina amesema ufadhili huo unakuja kupitia mchezo wa Ready.
"Tumeanza na kata ya Duga na leo kata ya Nguvumali ambayo imeshirikisha jumla timu 20.katika Bonanza hilo "alisema Meneja masoko huyo wa jiji la Tanga Mgina.
Kwa mujibu wa Meneja masoko Mgina, huko katika kata ya Nguvumali ,mchezo wa Ready ulioifanyika shule ya Gofu juu na aliueibuka mshindi ni timu ya Dadas alizawadiwa tsh. 70,000/-.
Mshindi wa pili katika michezo hiyo ni Nguvumali Princes aliyepata Shilingi 50,000/- na washindi wengine ni Sophia Yohana aliyeibuka mshindi kukuna Nazi.
Washindi wengine ni yule aliyepatikana kwa kunywa Soda Hassan Juma,kutoka chuo Cha fundi Veta,,kukuna nazi ni Sophia Yohana,kula Ndizi Joving Swai kutoka chuo Cha Veta ambayo wamepata pesa tasilimu.
Mwisho.










No comments:
Post a Comment