Tuesday, 8 September 2015

JINSI NSSF ILIVYOZIPIGA JEKI VILABU VYA SOKA MKOANI TANGA,,

 Mkono wa kushoto ni mkurugenzi wa NSSF taifa,Dkt.Ramadhani Dau akimkabizi mchezaji wa timu ya Coastal Union ya jijini Tanga cheki ya million 25 juzi uwanja wa Mkwakwani alipotembelea pambano la karne dhidi ya African Sports ambapo matokeo Coastal Union ilitoka kwa ushindi wa bao 1-0.
 Pichani mkono wa kushoto aliyevaa fulana ya mistari na miwani ni mkurugenzi mkuu wa NSSF taifa,Ramadhani Dau mara baada ya kumkabidhi cheki ya million 25,mchezaji wa timu ya Arican Sports akitoa maelekezo.
 Pichani ni mkurugenzi mkuu NSSF taifa,Dkt.Dau akiteta kitu na meneja wa NSSF mkoa wa mkoa wa Tanga,Dkt.Frank Maduga ambaye amevaa fulana ya njano mkono wa kulia juu ya zawadi za washindi .
Hizi ni zawadi zilizotolewa kwa timu za soka wanaume na wanawake juzi mkoani Tanga.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TIMU ya soka Wasichana wa shule ya Sekondari Kwamkabala Wilayani Muheza wameibuka mabingwa wa soka wa kombe la Mfuko wa Hifadhi ya jamii (NSSF) baada ya kuifunga Mang'enya bao 1-0.

Wakicheza katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Mkwakwani na
kushuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Ramadhani Dau  Kwamkabala iliwachukua dakika 40 kupata ushindi.

Bao hilo pekee lilifungwa na Sei Mnubi aliyewapiga chenga walinzi wa
Mang'enya Sekondari waliokuwa wamejaa  golini na hivyo kumchanganya
mlinda mlango Sauda Juma.

Kwa ushindi huo,Kwamkabala ilizawadiwa kombe,na seti ya sare na mpira wa soka huku Mang'enya na Mkwakwani ya Tanga ikijipatia mpira na sare za kuchezea soka.

Kwa upande wa soka la wasichana shule za msingi,Changa ilitoka sare ya
kufungana bao 1-1 na Chumbageni na hivyo kuzawadiwa sare pamoja na
mpira mmoja kwa kila timu.
Hata hivyo timu zote shiriki ambazo zimejitokeza kushiriki michuano hiyo  zimepatiwa jezi na mpira mmoja ili kupunguza ukata wa vifaa vya michezo kwa timu..

Meneja wa NSSF mkoa wa Tanga,Dkt.Frank Maduga mara baada ya kutoa zawadi kwa timu zilizoshiki alisema kuwa lengo NSSF iliamua kuendesha michuano hiyo ili kuwapa nafasi kwa kada ya wasichana kuibua vipaji vyao katika soka.
Alisema kwamba ni endelevu ambapo yalianza mwaka jana kwa kushirikisha timu za wasichana huku lengo kubwa kuweza kutoa elimu na kuibua na kuendeleza vipaji kwa kada hiyo.
Dkt.Maduka amesema mwaka huu yameweza kuleta hamasa kubwa pale walipowashirikisha timu za shule za msingi ambapo zote zimefanikiwa kupata zawadi ya vifaa vya michezo.

Hata hivyo kwa msimu huu mashindano hayo yalishirikisha timu sita za shule ya msingi mbili na sekondari nne ambazo ni shule ya sekondari Kwamkabala,Mang"enya,Mkwakwani,Usagara,Chumbageni na Changa kutoka wilaya ya Tanga na Muheza.
  Mwisho.

No comments:

Post a Comment