Kikosi hicho cha Fair Play Queens kinatarajiwa kuondoka
Jijini Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam mahali ambapo Premier League
inafanyika.
"Tunaendelea na mazoezi makali chini ya kocha wetu Idd Kuha
na kwa jinsi anavyowanoa wachezaji niseme tu hali sio mbaya, tunaamini
tutafanya vizuri "alisema Sophia Wakati msemaji wa kikosi cha timu ya
Fair Play Queens.
Hata hivyo msemaji huyo wa kikosi cha Fair Play Queens
alitoa wito kwa wadau wa mchezo wa Soka kujitokeza kwa wingi kufadhili
timu zinazowahusu Wanawake kutokana na mwamko wa wananchi kuzisaidia
kuwa mdogo.
Amesema, kitendo cha wadau kujitokeza kufadhili mchezo huo
kwa kada ya Wanawake kutaamsha ari ya wachezaji kufanya vyema jambo
ambalo pia litaibua ajira kwa jinsia hiyo.
Ligi hiyo ya Taifa Wanawake inatarajia kuanza kutimua vumbi
hapo Nov 27 mwaka huu ambapo awali itakuwa katika mtindo wa makundi
miwili.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa msemaji huyo wa Fair Play
Queen katika kundi lao litakaokipiga Jijini kuna timu za Simba Queen,
JKT, Mlandizi, Mburahati na Ever Green na kituo kingine kunakuwepo huko
Jijini Arusha.
Kapteni msaidizi wa timu ya Fair Play,Cristina Fransis
'Kazola' juzi uwanja katika mahojiano na Mwandishi wa makala haya
amejinasibu kwamba kikosi chake kiko imara kuivaa Simba Queen katika
mchezo wa ufunguzi.
Kazola amesema, kwa mazoezi waliyoyapata kupitia mwalimu
wao Kuha ni dhahiri kwamba wamepata mbinu za ziada kuwasambaratisha
wapinzania wao hao Simba Queens kwenye mchezo wa ufunguzi hivyo kujiweka
vyema.
Amesema,kwa mwaka huu wamejipanga kuibuka mabingwa wa ligi
hiyo ingawa alisema kupata ushindani kutoka kwa wapinzania wao itakuwa
jambo la kawaida kwa vile hakuna atakayekubali kupoteza mchezo kirahisi.
"Ushindani tunaamini ya kuwa utakuwepo ila kwetu sisi
hatuendi kutembea inahitaji bingwa tukianza kuusaka katika mchezo wetu
wa ufunguzi "alisema Kazola.
Katika taarifa yake kwa gazeti hili meneja wa Fair Play
Queen Khalid Abdallah alisema kikosi chake kitaondoka Jijini Tanga
wakati wowote kuanzia sasa (23/11/2017)ili kuweka kambi ya mazoezi
kuzoea mazingira huko Jijini Dar es salaam.
Alisema, viongozi watakaoambatana na timu hiyo licha ya
wachezaji wote ni mwalimu Idd Kuha, datari wa timu, kocha msaidizi na
Mwisho.
Pichani mkono wa kushoto amesimama ni mkurugenzi wa vikosi hivyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Coastal Union ,Khald Abdallah juzi mara baada ya mazoezi akiwapa maelekezo na mbinu mbalimbali za mchezo huo uwanja wa soka D'Souza jijini Tanga.
Pichani mkono wa kushoto amesimama ni mkurugenzi wa
vikosi hivyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Coastal Union,Khald
Abdallah akiwapa maelekezo na mbinu mbalimbali za mchezo huo uwanja wa
soka D'Souza jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment