Waziri Jaffo alitoa
agizo hilo jana alipokuwa akipokea taarifa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga kwa ziara ya kikazi akisema kuwa ulipaji
wa fedha hizo za vijana na wanawake ni agizo la serikali kupitia chama tawala
akisistiza kusema kuwa tayari fedha hizo zilishatengwa kwa kada hiyo.
Alisema
katika agizo hilo utekelezwaji wake umekuwa mdogo ambapo mpaka sasa kuna baadhi ya
halmashauri bado hazijatekeleza adhima hiyo ikiwa ni moja ya mkakati wa serikal na ilani ya chama cha mapinduzi.
Akionyesha msisitizo juu
ya fedha hizo za vijana na wanawake,Waziri Jaffo alisema kuwa iwapo wahusika
watapatiwa stahili hiyo itakuwa rahisi kwao kupata mitaji na hivyo kuendesha
shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuondokana na hali tegemezi hapa nchini.
“Viongozi fedha hizi
zipo na tayari zilishatengwa na serikal,kila halmashauri imnapewa mil 61.5
hivyo kila halmashauri inatakiwa kuhakikisha kwamba hadi kufikia mwakani iwe
imeshalipa asilimia kumi (10%) ya fedha za wanawake na vijana”alisema Waziri huyo
Suleiman Jaffo.
Aidha,Pia ameliagiza
Jiji la Tanga kuhakikisha kwamba inawatengea eneo maalum mafundi cherahani ili
kuweza kuendesha shughuli zao kwa tija ambapo alisema kuwa kwa kufanya hivyo
itasaidia kukuza ajira miongoni mwa jamii hasa kada ya vijana.
Mbali na hayo katika
mazungumzo yake wakati akipokea taarifa ya mkuu wa wilaya ya Tanga,Waziri Jaffo
alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi kuendelea kuchapa kazi kwa kujituma
hatua aliyoieleza kuwa itasaidia kuiwezesha serikali kufikia malengo yake.
Awali mkuu wa wilaya ya
Tanga,Thobias Mwilapwa katika taarifa yake alimweleza Waziri Jaffo kuwa Tanga
imetenga maeneo ya viwanda huko Kiomoni ekari 101 na Mabokweni ekari 117 hatua
ambayo ilipongezwa na Waziri huyo wa Tamisemi.
Katika pongezi zake hizo
Waziri Jaffo alisema amefurahishwa na hatua hiyo ya Tanga kuunga mkono agizo la
serikal kutenga maeneo huku akitanabaisha kuwa kimkakati Tanga ni miongoni mwa mikoa
ya viwanda ambapo kunahitajika uwepo wa viwanda vidogo na vile vya kati ili
kukuza uchumi.
Naye mkurugenzi wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga,Dudi Mayeji alieleza kuwa wamefanikiwa kufanya
marekebisho kwenye barabara zake na hivyo kuwezesha miundombinu hiyo kuwa
kwenye ubora na kulifanya Jiji kurejea hadhi yake .
Katika ziara hiyo baadhi
ya maeneo ambayo ametembelea Waziri huyo wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na
serikali za mitaa ni kituo cha Televisheni ya jamii TaTv,eneo la Pongwe kwenye
shule yenye watoto wenye mahitaji maalum,shule ya msingi Kiomoni kuweka jiwe la
msingi,shule ya msingi Bombo kukagua maendeleo ya ujenzi na kukagua dula la
dawa la jamii.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment