Sunday 3 December 2017

UCHAGUZI WA CCM KUWAPATA VIONGOZI WA MKOA WA TANGA ULIKUWA HIVI,,

 Pichani ni msimamizi wa uchaguzi wa CCM Mkoa wa Tanga kutoka makao makuu ya CCM taifa,Steven Kazidi akiwaeleza wajumbe kanuni zinaelekeza uchaguzi huo una kila sababu za kurudiwa kwa nafasi ya mwenyekiti kwa vile mshindi alitakiwa kupata idadi ya nusu ya kura au zaidi. 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi CCM wamemchagua,Henry Daffa Shekifu kuwa Mwenyekiti wao wa kuwatumikia miaka mitano mkoani Tanga katika kinyang'anyiro cha uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali.


Uchaguzi huo uliofanyika juzi (2/12/2017) ulianza saa Saba mchana na hatimaye matokeo kutangaza saa 11 alfajiri ya 3/12/2017 katika ukumbi wa chuo kikuu cha Eckenford jijini hapo.
Waliokuwa wakiwania nafasi ya mwenyekiti ni Balozi Abdi Mshangama,Mohamed Rished na Henry Daffa Shekifu aliyekuwa akitetea wadhifa wake.

Katika hatua za awali za uchaguzi huo Mohamedi Rished alipata kura 133,Henry Daffa Shekifu kura 528 na Balozi Abdi Hassan Mshangama alipata kura 600.

Hata hivyo kwa matokeo hayo,msimamizi wa uchaguzi huo kutoka makao makuu ya CCM taifa,Steven Kazidi alisema kanuni zinaelekeza uchaguzi huo kurudiwa kwa nafasi ya mwenyekiti kwa vile mshindi alitakiwa kupata idadi ya nusu ya kura au zaidi. 

Uchaguzi wa marudio uliowahusisha Wagombea wawili ambao ni Henry Daffa Shekifu na Balozi Abdi Mshangama kura zikiwa zilianza kupigwa saa nne usiku. 

Hata hivyo katika uchaguzi huo uliokuwa wa vuta nikuvute Balozi Mshangama alipata kura 530 na Shekifu alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 609.

Msimamizi wa uchaguzi huo Steven Kazidi akimtangaza Henry Daffa Shekifu kuwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga huku akiueleza uchaguzi huo kuwa ulikuwa niwa aina yake kufanyika hapa nchini. 

Kwa upande wao wagombea akiwemo Mohamedi Rished alieleza kuridhishwa kwake na zoezi la matokeo hayo akiwasihi Wanachama kuimarisha mshikamano jambo ambalo pia liliungwa mkono na Shekifu akionya uwepo wa mipasuko ndani ya chama hicho. 

Uchaguzi huo pia uliwezesha kupatikana kwa wajumbe 18 ambapo kila halmashauri ya wilaya walitoka wajumbe wawili kuwa wawakilishi wa mkutano wa halmashauri kuu ya mkoa.

Aidha,mwanachama wa CCM Mohamedi Salim Said (RATCO)  ameukwaa ujumbe wa NEC Taifa kwa kupata kura 701 akiwabwaga John Raphael Nyika kura 48,Dk.Najim Zuberi Msenga kura 437 na Profesa Cathbert Mhilu kura 42.

Awali katika uchaguzi huo chama cha mapinduzi CCM kilimpokea aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA,Frenk Shempemba na David Chanyeghea aliyerejea CCM akidai kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli. 

Chanyeghea katika uchaguzi uliyopita aliwania ubunge Jimbo la Bumbuli kupitia CHADEMA akichuana na Waziri January Makamba wa chama tawala CCM.
Mwisho.
 Zoezi la uchaguzi mkoa wa Tanga lilikuwa hivi,,

 Miongoni mwa wajumbe.
 Pchani mkono wa kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi akimtambulisha mwanachama mpya Devid Chanyeghea kutoka CHADEMA mara baada ya kurudisha kadi na kujiunga na CCM.
 Pichani mkono wa kulia ni aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Bumbuli kupitia CHADEMA,Devid Chanyeghea mara baada ya kurudisha kadi na kujiunga na CCM,akiwa Frenk Shempemba wote kutoka CHADEMA wakibadilishasha mawazo nje ya ukumbi wa Eckenford wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa CCM.
 Pichani mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga,Henry Shekifu mara baada ya kutangazwa mshindi akiwataka wajumbe kushirikiana kuondoa mipasuko ndani ya chama hicho ili kuimarisha ngome ya CCM.
 Pichani ni mwanachama wa CCM Mohamedi Salim Said maarufu (RATCO)  mara baada ya kuukwaa ujumbe wa NEC Taifa kwa kupata kura 701 kwa kuwabwaga wapinzani wake John Raphael Nyika kura 48,Dk.Najim Zuberi Msenga kura 437 na Profesa Cathbert Mhilu kura 42.
Pichani ni katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kabla ya zoezi la uchaguzi akitoa maelekezo kwa wajumbe wenye sifa ya kupiga kura kuwapata viongozi wa ngazi ya mkoa huo.

No comments:

Post a Comment