Pichani ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Kamishna msaidizi
mwandamizi,Edward
Bukombe Selestin akizungumza na Waandishi wa
habari ofisini kwake (hawapo pichani) na kujitambulisaha ambapo amesema kuelekea kumaliza mwaka 2017,hali ya uhalifu mkoani hapo ni amani na utulivu huku akibainisha mkakati uliopo kudhibiti
vitendo vya uhali katika kusheherekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya.
NA SOPHIA WAKATI, TANGA
KATIKA
kusherehekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, jeshi la Polisi Mkoani
Tanga limewataka Wamiliki wa kumbi za starehe kuzingatia sheria iliyopo
ili kuepuka kubugudhi watu wengine.
Licha
ya kutoa rai hiyo kwa wamiliki kumbi za starehe pia jeshi hilo
limewataka wananchi kujiepusha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa
amani kama milipuko ya baruti na fatalities.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga Kamishna msaidizi mwandamizi,Edward Bukombe
Selestin ametoa wito huo LEO wakati akizungumza na Waandishi wa habari
ofisini kwake na kujitambulisaha na kueleza kuhusiana na hali ya ulinzi
na Usalama kuelekea kumaliza mwaka.
Akizungumzia
kumbi za starehe Kamanda,Selestin alisema, wamiliki mkoani hapo
wanapaswa kuzingatia sheria inayodhibiti mtu kufanya shughuli zake bila
bugudha kwa wengine.
Aidha Kamanda
huyo alisema, sheria ya kumbi za starehe za Usiku 'Night Club'ziko wazi
zikielekeza shughuli zote kufanyika ndani huku alitanabaisha kuwa Bar
na sehemu nyingine Mwisho wao unatakiwa kuwa saa tano usiku.
Kuhusu
milipuko, alisema kuwa mtu kujihusisha na vitendo hivyo ni kinyume cha
sheria namba 13 ambapo adhabu yake ni faini shilingi milioni tano,
kifungo miaka mitatu au vyote viwili kwa pamoja.
Kamanda
Selestin alitumia fursa hiyo kutoa msisitizo kwa maeneo ya nyumba za
Ibada akiwataka viongozi wake kuhakikisha wanaendesha Ibada kwa muda
muafaka ili kuepuka mkanganyiko.
Kamanda
huyo wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga Kamishna msaidizi mwandamizi,Selestin amebainisha kuwa kipindi cha kuanzia mwenzi January
hadi Novemba 2017 jumla ya matukio ya uhalifu 16799 yameripotiwa tofauti
na mwaka jana 17548.
Pia
amebainisha kwamba jeshi la polisi katika kipindi hicho limefanikiwa kuendesha misako na
operesheni katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kukamata wahalifu na
vielelezo vya kesi ikiwemo bhangi yenye uzito wa kilogramu 761.1,huku
kesi 37 zimefunguliwa.
Huku
mirungi yenye uzito wa kilogramu 5396,740 zilikamatwa,madawa ya kulevya
ya viwandani jumla ya kesi 55 zimefunguliwa baada ya uzito wa kilogramu
3.749 kukamatwa.
Kwa upande wa
kudhibiti wahamiaji haramu 224 walikatwa kipindi hicho cha January hadi
Novemba 2017 huku wasomali wakiwa 55,waEthiopia 149 na raia wa nchi
jirani wa Kenya wakiwa 20.
Kamanda,
Selestin ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa jamii kuendelea
kushirikiana na jeshi hilo kupeana taarifa hatua ambayo itachangia
kudhibiti vitendo vya uhalifu katika mkoa mzima wa Tanga.
"Kiukweli
kipindi hiki cha kuelekea msimu huu wa sherehe za sikukuu za krismasi
na mwaka mpya jeshi la polisi limejipanga kuimarisha hali ya ulinzi na
Usalama wakati wote huo"alisema kamanda Selestin.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment