Sunday 19 November 2017

ZOEZI LA BALOZI WA KUWAIT NCHI TANZANIA,JAASIM KUKABIDHI KISIMA NA VIFAA KWA AJILI YA MAMA NA MTOTO ILIKUWA HIVI,,

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
SERIKALI ya Kuwait imesema itaendelea kumuunga mkono Rais wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli kwa adhima yake ya elimu bure kwa kusaidia sekta ya elimu na afya hapa nchini.

Hata hivyo,imesema itasaidia kutekeleza ujenzi wa miradi ya maji mashuleni na hospitali ya wilaya ya Tanga, katika eneo la Tangasisi ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano katika kuboresha huduma za afya hapa nchini.
 
Akizungumza jana katika hafla akikabidhi kisima cha maji shule ya sekondari Old Tanga na vifaa vya mama na mtoto katika kituo cha afya cha Ngamiani Jijini hapa, balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaasim Alnaajim.

Alisema ujenzi huo na misaada waliyotoa ni miongoni mwa matokeo ya maombi waliyopewa na Makamu wa Rais wa Tanzania,Samia Saluhu kuwasaidia katika sekta ya afya na elimu.

Aidha alisema mbali na msaada huo wa kisima ambacho kigharimu million sita za kitanzania,pia watasaidia ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya  iliyokuwa katika mpango wa halmashauri ya jiji la Tanga ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya mkoa huo ya Bombo ambayo ni ya rufaa katika mkoa huo wa Tanga.

“Kiukweli nchi yetu imegushwa na itasaidia ujenzi huo wa hospitali ya wilaya kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta ya afya ili kuisaidia jamii ya Watanzania,”alisema Balozi huyo Alnaajim.

Balozi huyo aliyekuwa ameongozana na viongozi wa taasisi ya African Muslim Agency, Mohamed Abas awali akikabidhi kisima katika shule ya sekondari Old Tanga ambapo pia ameaahidi kuwapa kompyuta mbili, kisha baadaye alisaidia vifaa vya mama anapojifungua ikiwemo beseni la kumuogesha mtoto.

Alisema misaada hiyo imetolewa na wananchi wa Kuwait pamoja na shirika la Mwezi Mwekundu ambalo limetoa vifaa hivyo vipatavyo 42 katika kituo hicho cha afya na ameaahidi kusaidia kadiri watakavyoweza.

Balozi huyo alibainisha kuwa nchi yake tayari imesaidia shule na vituo vya afya katika wilaya mbalimbali hapa nchini akizitaja za Mkulanga, Iringa na wilaya za Dar es salaam mpango ambao wataendelea kusaidia katika sekta hizo kadiri watakavyopata mahitaji.

Meya wa Jiji la Tanga,Muhina Mustapha maarufu  'Seleboss', aliyekuwa na Mkurugenzi wa Jiji, Daud Mayeji, aliushukuru ubalozi huo kwa masaada huo na akamuomba pia aweze kusaidia katika shule nyingine za Jiji hilo zipatazo 98 za msingi na sekondari 32 lakini pia aliomba kusaidiwa jengo la mama na mtoto wanalotarajia kulijenga Ngamiani kwa gharama za dola za Kimarekani Milioni 5.
akiwa na mwenyekiti wa bodi ya shule,Kassim Kisauji,meya wa jiji la Tanga,Muhina Mustapha Seleboss mkono wa kulia.
  Pichani mkono wa kulia balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaasim Alnaajimmara baada ya kufungua mradi wa kisima kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Old Tanga na kunywa maji hayo akimkabidhi meya wa jiji la Tanga,Muhina Mustapha Seleboss kushoto ambaye amevaa joho la ugoro

 Pichani mkono wa kulia balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaasim Alnaajimmara baada ya kufungua mradi wa kisima kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Old Tanga na kunywa maji hayo akimkabidhi mkurugenzi wa jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ambaye amevaa suti ya bluu.

 Pichani ni mkono wa kushoto ni balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaasim Alnaajim akimkabidhi vifaa meya wa jiji la Tanga,Muhina Mustapha Seleboss kwa ajili ya mama na mtoto kituo cha afya Ngamiani

 Pichani mkono wa kulia ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Ngamiani Jijini Tanga, akimkabidhi balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jaasim Alnaajim moja ya watoto waliozaliwa usiku wa kuamkia juzi.



Mwisho

No comments:

Post a Comment