Wednesday 21 March 2018

JINSI KAMPUNI YA KATANI ILIVYOJIPANGA KUJITANGAZA KUPITIA SEKTA YA MICHEZO,,

Pichani ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Katani,Juma Shamte mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya million 7 kwa ajili ya kuingia udhamini wa mashindano ya 'Tanga City Marathon 2018' akieleza malengo yaliyopo.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KAMPUNI ya Katani Limited yenye makao makuu yake Jijini Tanga, imesema ina mpango wa kuwa miongoni mwa wadhamini wa klabu ya Coastal Union ili kuweza kufanya vizuri michuano ya ligi kuu msimu ujao Tanzania bara.

Hata hivyo,imesema kadiri itakavyokuwa na uzalishaji wa kiwango cha juu katika malighafi inayotokana na zao la Mkonge,itaidhamini moja kwa moja klabu hiyo ya Coastal Union inayoshiriki Ligi ya Vodacom.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana,mara baada ya kutangaza kuingia udhamini wa mashindano ya 'Tanga City Marathon 2018',Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Juma Shamte,.

Alisema kuwa lengo la kujiingiza kwenye michezo ni njia mojawapo ya kuhamasisha ulimaji wa zao la mkonge kwa wakulima na wanunuzi wa bidhaa inayotokana na zao hilo ndani na nje ya nchi.

Alibainisha kuwa kadiri watakavyoweza kukua na kuzalisha kwa wingi bidhaa zitokanazo na mkonge, wataweza kuwa na fursa zaidi ya kujiingiza katika michezo na kwamba wanaweza kukutana na viongozi wa Coastal wakatazama kama wanaweza na wao kuifadhili.

"Kiukweli kadiri tunavyokuwa na kuzalisha tutaweza kutoa fursa zaidi za kujiingiza katika michezo ni suala la kufanyia kazi kama tunaweza, kukutana na viongozi wa Coastal kuangalia ni jinsi gani tunaweza kushiriki " alisema Shamte.

Shamte alisema kampuni hiyo ambayo ina mashidnano yake ya endelevu kila mwaka yanayofahamika kwa jina la 'Mkonge Cup' kwa kushirikisha timu mbalimbali za madaraja ya chini.

Hata hivyo,kampuni hiyo imekabidhi hundi ya shilingi milioni 7 kwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo yatafanyika Machi 31 na jumla ya washiriki 500 hadi sa sa wamejiandikisha kushiriki mbio hizo.

Alisema aliongeza kuwa kadiri watakavyoweza kukua na kuzalisha kwa wingi bidhaa zitokanazo na mkonge, wataweza kuwa na fursa zaidi ya kujiingiza katika michezo na kwamba wanaweza kukutana na viongozi wa Coastal wakatazama kama wanaweza na wao kuifadhili.

"Kiukweli kadiri tunavyokuwa na kuzalisha mzuri tutaweza kutumia fursa zaidi za kujiingiza katika michezo,kwa kukutana na viongozi wa Coastal ili kuangalia tunashiriki vipi," alisema.

Shamte alisema kuwa lengo kubwa ni kusaidia timu mbalimbali za madaraja ya chini ili kuweza kuibua vipaji na kujitangaza kupitia sekta hiyo ya michezo.

Hata hivyo,kampuni hiyo imekabidhi hundi ya shilingi milioni 7 kwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo yatafanyika Machi 31 na jumla ya washiriki 500 hadi sasa tayari wamethibitisha kushiriki mbio hizo.

Nae Mratibu wa mashindano hayo,Juma Mwajasho alisema kwamba mashindano hayo yatashirikisha mbio ndefu kilomita 21,10 pamoja na mbio fupi za kilomita 5 ambazo mara nyingi ni za watu wa aina mbalimbali kukimbia kama kujifurahisha. Mwisho.

No comments:

Post a Comment