Thursday 29 March 2018

Mashindiano ya mbio za 'Tanga City Marathoni Nusu 2018,yalivyoboreshwa msimu huu,,

 Pichani katikati  ambaye anaongea ni mratibu wa mashindano ya Mashindiano ya mbio za 'Tanga City Marathoni Nusu 2018,Juma Mwajasho akizungumzia juu ya washiriki 600 ambao tayari wameshathibitisha kushiriki mbio hizo.
 Pichani katikati mratibu wa mashindano ya Mashindiano ya mbio za 'Tanga City Marathoni Nusu 2018,Juma Mwajasho akionyesha baadhi ya medani ambazo zitatolewa kwa washiriki wa mbio hizo.
 Pichani katikati ni miongoni mwa mdhamini msemaji kutoka Nyumbani Hoteli,Benjamin Mosha,akizungumzia kwa upande wa malazi ya wageni watakaowasili mkoani Tanga katika  Mashindiano ya mbio za 'Tanga City Marathoni Nusu 2018.
Pichani katikati ambaye anaongea ni katibu wa chama cha riadha mkoani Tanga,Hassan Tuano akizungumzia maboresho mbalimbali ikiwemo ya njia zitakazotumika kwa washiriki  mbio za 'Tanga City Marathoni Nusu 201.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WADHAMINI wa Mashindiano ya mbio za 'Tanga City Marathoni Nusu 2018 zenye kilomita 21 na 10  zitakazofanyika Machi 31 mwaka huu Jijini Tanga, wamesema zawadi kwa washindi zimeboreshwa.


Mdhamini wa mashindano hayo Meneja Mkuu wa kampuni ya Mkwabi Group ya Jijini Tanga, Kawkab Hussein akizungumza na Waandishi wa Habari jana, alisema kuwa mchakato ikiwemo zawadi kwa washindi wote watakaoshiriki mbio hizo zipo tayari.


Alisema mshindi wa kwanza kwa mbio za kilomita 21, upande wa wanawake na wanaume, atapata kitita cha sh. 700,000, mshindi wa pili sh. 500,000, wa tatu sh. 300,000 huku wa nne hadi wa kumi wakipata kifuta jacho cha sh. 50,000.

Kawkab alisema kwamba mbio za kilomita 10, mshindi wa kwanza atapata kiasi cha sh. 250,000, wa pili sh. 150,000, wa tatu sh. 100,000 huku mshindi wa nne hadi kumi wakipata kifuta jasho cha sh. 30,000 kila mmoja.


Mratibu wa mashindano hayo, Juma Mwajasho alibaini kueleza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na idadi kubwa ya washiriki ambapo  mpaka sasa waliojiandikisha imefikia 600 na wamesogeza mbele  zoezi la kujiandikisha hadi Ijumaa jioni.

Kwa upande wake katibu wa Chama Cha Riadha mkoani Tanga (RT),Hassain Tuano alisema mbio za mwaka huu zimezingatia ubora wa Kimataifa baada ya njia watakazopita wanariadha hao, zimepimwa na mtaalamu anayetambulika na vyama vya RT na IFF,John Bayo.


"Kiukweli mbio za mwaka huu zitakuwa zinatambulika Kimataifa baada ya kumtumia mtaalamu John Bayo anayetambulika na shirikisho letu na lile la Dunia IFF,pia tumepata wanariadha wageni kutoka Seychellys na Zanzibar," alisema Tuano.

Miongoni mwa wasemaji wa wadhamini wa kampuni ya Katani Limited na Nyumbani Hoteli, Fatuma Nyombi na Benjamin Mosha,walisema kwamba mashindano hayo yataleta hamasa kubwa na kuendeleza na kufufua vipaji vya mchezo huo mkoani Tanga.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment