Pichani ni mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Tanga,Said Soud akizungumzia furaha yake kwa timu hiyo kupanda daraja,
Pichanikatikati mwanamke ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalim mara baada ya kukabidhi eneo la michezo kwa uongozi wa timu ya Coastal Union kama furaha yake baada ya timu hiyo kupanda daraja,akiwa na viongozi na baadhi ya wanachama wa timu hiyo.
Pichanikatikati mwanamke ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalim mara baada ya kukabidhi eneo la michezo kwa uongozi wa timu ya Coastal Union kama furaha yake baada ya timu hiyo kupanda daraja.
Pichanikatikati mwanamke ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalim mara baada ya kukabidhi eneo la michezo kwa uongozi wa timu ya Coastal Union kama furaha yake baada ya timu hiyo kupanda daraja.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
UONGOZI
klabu ya Coastal Union yenye maskani yake barabara ya 11 Jijini Tanga
imesema itamuunga mkono na kuwa naye bega kwa bega Mbunge wa Viti
maalum Mkoani Tanga, Ummy Mwalimu katika harakati zake zote za
kuwaletea Maendeleo wananchi wa Tanga.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa mpito wa klabu hiyo,Stephen Mnguto
wakati akishukuru kwa kukabidhiwa eneo ambalo watakalojenga uwanja wa mpira wa klabu hiyo.
Alisema
kuwa Kitendo alichofanya mbunge hyo Ummy kuwapa eneo watakalojenga
uwanja ni jambo kubwa lililoandika historia ya klabu hiyo tangu
ianzishwe Mwaka 1948.
"Kiukweli
mheshimiwa hili ulilotufanyia umetujengea heshima kubwa kwa klabu yetu
na sisi kulipa fadhila tunakuahidi tutakuunga mkono kwa jambo lolote la
maendeleo utakalolifanya lenye maslahi kwa watu wa Tanga, "alisema
Mnguto.
Eneo
hilo lililopo mtaa wa Kichangani kata ya Maweni Jijini hapa linaukubwa
wa mita za mraba zipatazo 7,632 yenye thamani ya sh. 38,160,000 ambalo
limetolewa na mbunge huyo kwa kushirikiana na kampuni ya City Plan ya
Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa kampuni ya City Plan Dk. Juma Mohamed alisema eneo hilo wamelitoa
kwa klabu hiyo baada ya kuombwa na Ummy kwa ajili ya kujengwa uwanja wa
kisasa wa mpira wa miguu wa Coastal.
Hata
hivyo, Dk. Mohammed alisema baada ya kutenga eneo, waliacha wazi eneo
jingine lililipo jirani na kiwanja hicho lenye ukubwa wa mita za mraba
zipatazo 9,0000 zenye thamani ya sh. 48,000,000 kwa ajili ya kujengwa
hosteli za wachezaji wa timu hiyo vyumba vya kufanyia mazoezi ya viungo.
Kuzungumza
katika hafla hiyo fupi iliyofanyikia eneo la uwanja huo na kuhudhuriwa
na mashabiki kadhaa kikiwemo kikundi cha ngoma cha timu hiyo, Ummy
ambaye pia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, alisema amekabidhi kiwanja hicho kama furaha yake baada ya timu
hiyo kupanda daraja.
Aidha,alisema
baada ya timu kupanda daraja pia aliahidi kuiletea maendeleo ili timu
hiyo iweze kushiriki Ligi Kuu kwa mafanikio na kuiletea heshima mkoa wa
Tanga kupitia michezo.
"Nawapongeza
sana City Plan kwa kuunga mkono jitihada zetu za kuindeleza Coastal
Union, kilichobaki tuzidi kushikamana ili tuweze kufanya vizuri zaidi,
"Alisema Ummy.
Waziri
huyo aliahidi kutafuta fedha nyingine kiasi cha Shilingi milioni 48 ili
aweze kuchukua eneo jingine lenye viwanja 16 kwa ajili ya kujengwa
hosteli ya klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Mkuu
wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa alimpongeza Waziri Ummy kwa
jitihada zake za kuisaidia timu hiyo ambayo kupanda kwake daraja
kulitokana na jitihada zake za kurudisha umoja uliokosekana kwa klabu
hiyo hapo awali.
Nae
Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoani Tanga (TRFA) Said Suod
alimpongeza Waziri Ummy kwa hatua ya kufanikisha kupatikana uwanja huo
kwa klabu hiyo baada ya kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake lakini
haukuwa na uwanja wake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment