Monday 12 March 2018

 Kamanda wa polisi mkoani Tanga,akiwaonyesha waandishi wa habari gari aina ya RAV 4 iliyotumika kufanya unyang"anyi wa kupora million 7 jijini Tanga,
  Kamanda wa polisi mkoani Tanga,akiwaonyesha waandishi wa habari gari aina ya RAV 4 iliyotumika kufanya unyang"anyi wa kupora million 7 jijini Tanga,
  Pichani ni gari aina ya RAV 4 iliyotumika kufanya unyang"anyi wa kupora million 7 jijini Tanga,
 Pichani ni gari ya wizi iliyokamatwa katika doria na jeshi la polisi jijini Tanga.
 Pichani ni sare ya polisi,redio Cool,bastola ya bandia na kamba vilivyotumiwa na wahalifu kwenye tukio la unyang"anyi wa million 7 jijini Tanga.
Pichani ni bidhaa mbalimbali za magendo zilizokamatwa na jeshi la polisi jijini Tanga.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la polisi linawashikilia watu watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bastola bandia,redio cool ambayo bado haijajulikana niya kampuni gani katika kizuizi cha polisi Kabuku kilichopo wilayani Handeni, baada ya kufanya tukio la uhalifu Jijini Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polii Mkoani Tanga, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Edward Bukombe alisema tukio hilo limetokea Machi 11 mwaka huu,mtaa wa Magaoni ambako watu watano wanaohisiwa kuwa majambazi walivamia
nyumbani kwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Allen Daud na kuiba million saba na vifaa mbalimbali.

Alisema watu hao baada ya kuvamia nyumba hiyo walijitambulisha kwamba wao ni maofisa wa polisi, kisha ghafla wakawaweka chini ya ulinzi wapangaji watatu waliokuwa wakiisha katika nyumba hiyo na kuwafunga kamba miguuni na kuwaziba midomo kwa kutumia plasta.

Aliwataja wapangaji hao ambao walikutwa sebuleni na majambazi hayo saa 7.30 mchana, kuwa ni pamoja na Grace Daud (32), David Ngilisho (49) ambaye ni mwalimu na Lazaro Benjamin (25).

Kamanda,Bukombe alisema watu hao, mmoja akiwa amevalia sare ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walifika eneo hilo wakiwa katika gari aina ya Rav 4 yenye namba T 764 CKD huku mmoja akishika simu ya upepo 'Redio Call',  kama wafanyavyo askari wa ukweli na walikuwa na bastola bandia.

Alisema wakati wamewaweka chini ya ulinzi walifanikiwa kuiba kiasi cha fedha taslimu sh. 7,000,000, simu mbili aina ya Itel na Tecno pamoja na kompyuta mpakato 'Laptop' aina ya Dell.

"Majambazi hao mbinu waliyotumia kuiba,walijitambulisha kama askari na ghafla waliwaweka chini ya ulinzi wapangaji watatu na kisha kuwafunga kamba miguuni na kuwaziba midomo kwa plasta," alisema Kamnada huyo.

Kamanda,Bukombe alisema baada ya watu hao kufanikiwa kuiba waliondoka eneo hilo na taarifa kufikishwa kituo cha polisi Chumbageni ambao mara moja walianza kuwasaka na hatimaye saa 10:00 usiku huko wilayani Handeni kwenye kizuizi kilichopo katika mji mdogo wa Kabuku, walikamata.

Kamanda huyo,alisema wakati wanakamtwa washitakiwa wawili ambao hawakuwataja majina yao kwa sababu za kiupelelezi, walikimbia porini na wengine watatu pia majina yao hakuyataja, wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa ili kuwabaini mtandao wao wote.

"Kiukweli natoa wito, majambazi watafanikiwa kuja kwetu na kupanga njama za wizi, hilo watafanikiwa kwa sababu sisi hatutakuwepo eneo hilo, lakini wakishatekeleza na kuiba hawatafanikiwa kutoka salama, tumejipanga kukabiliana nao," alisema Kamnada Bukombe.


Mwisho.


No comments:

Post a Comment