Monday 27 December 2021

TIMU YA SOKA YA SHIRIKA LA UMEME PEMBA ZANZIBAR ZECO KATIKA ZIARA YAKE MKOANI TANGA 2021.ILIKUWA HIVI,,

 

Timu ya  Shirika la umeme Pemba Zanzibar ZECO na wapinzani wao Tanesco Tanga mara baada ya mechi ya kirafiki wakiwa kwenye picha ya pamoja katika uwanja wa Galanos jijini Tanga.

 Timu ya soka ya Shirika la umeme Pemba Zanzibar ZECO mara baada ya mechi katika ziara yao mkoani Tanga.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA

TIMU ya soka ya Shirika la Umeme Tanesco mkoani Tanga juzi imetoka kifua mbele baada ya kuifunga Shirika la umeme Pemba Zanzibar ZECO kwa magoli 3-1.

 Mchezo huo wa ujirani mwema kati ya timu za Shirika la umeme Zanzibar ZECO na Tanesco Tanga uliopigwa kwenye uwanja wa Galanosi uliopo Jijini Tanga.

 Katika vuta nikuvute ya mchezo Tanesco Tanga ilikuwa ya kwanza kufunga Magoli yake kupitia vinara wake Leanard Teve dakika ya 16 ,Kurwa Ally dakika ya 54 na HamzaJuma dakika ya  51.

Baada ya kuingia kwa magoli hayo kipindi cha pili cha mchezo huo Tanesco Pemba ilikuja ilijipanga kuonyesha kandanda ambayo yalileta mafanikio dakika ya 63 ilifanikiwa kusawadhisha goli moja kupitia Salehe Abdallah Kassim..

Katika mchezo wao wa kwanza kwenye ziara yao hiyo mkoani Tanga, ZECO waliwachapa Worrier ya jijini hapo kwa magoli 2 kwa 1,.

Magoli ya ZECO katika mchezo wake dhidi ya Worrier yalifungwa na vinara wa timu hiyo Omari Ramadhani Fadhil na Jamil Issa Ally dakika ya 27 na 41.

Afisa uhusiano wa shirika la umeme tawi la Pemba ZECO,Amos Salum
Masoudi alisema,lengo la ziara yao ni kujenga uhusiano hatua ambayo
husaidia kuleta ufanisi kazini.

Naye kiongozi wa kikosi cha Tanesco Tanga, Muhsin Mselemu alisema kwamba mchezo huo wa ujirani mwema ni muhimu  utasaidia kuboresha mahusiano kazini na kujenga undugu eneo la kazi.

Mwisho.


1 comment:

  1. Ni jambo jema kwa Tanesco kucheza na Jirani zao wa zeco kwani itasaidia kuongeaza uhusiano mwema na ufanisi katika kazi

    ReplyDelete