Sunday, 9 October 2022

BENKI YA AZANIA TAWI LA TANGA IMMETUMIA MILLION 1.4 KUTOA ZAWADI WODI TATU HOSPITAL YA RUFAA BOMBO,,,

Pichani ni Meneja wa benki Azania Tawi la Tanga, Hajira Mmambe,baada ya kukabidhi zawadi katika wodi tatu hospital ya rufaa Bombo mkoani hapo akieleza lengo ni sehemu ya kurudisha kile kilichopatika kutoka kwa wananchi.

 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

BENKI ya Azania tawi la Tanga imetumia wiki ya wateja kwa kutoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya sh 1.4 millioni za kitanzania kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya rufaa Bombo iliyopo Jijini Tanga.

Zawadi hizo zimetolewa juzi na Meneja wa benki hiyo, Hajira Mmambe,baada ya kukabidhi zawadi hizo alisema ni sehemu ya kurudisha kile kilichopatika kutoka kwa wananchi.

Alitaja katika wodi tatu za kina mama wajawazito na watoto wamewapatia wagonjwa hao Sabuni ya unga,sabuni ya miche na dempasi kwa ajili ya watoto wadogo.

Alisema kwamba hatua hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya kusherehekea wiki ya wateja kwa kurejesha fadhila kwa kile ambacho wamekuwa wakikipata .

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja,ni utamaduni wa benki ya Azania kugawana faida na wadau juu ya kile tunachopata"alisema Meneja huyo Mmambe.

Pia amewataka wadau wengine kuwa tayari kujitolea kwa wagonjwa  lengo likiwa kuwafariji kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali wawapo hospitalini wakiendelea kupatiwa matibabu.

Aidha,Mmande amesema benki yao imekuwa ikitoa huduma kama ilivyo kwa benki nyingine huku akiwasihi wananchi kutokusita kuitumia katika kupata huduma.

Mbali na hayo Mmande alidokeza kuwa,benki hiyo ya Azania inatoa mikopo kwa wajasiriamali waliojiunga vikundi na hata mtu mmoja mmoja huku akitanabaisha kuwa kabla ya kukopeshwa watapatiwa elimu.

Nae Muuguzi wa zamu hospitali ya rufaa bombo,Halima Rico alishukuru kwa msaada huo ambapo wagonjwa 41 kutoka wodi tatu wamenufaika na kuwataka wadau wengine kuiga utamaduni huo. 
Mwisho.

Pichani mkono wa kulia ni Meneja wa benki Azania Tawi la Tanga, Hajira Mmambe,akimkabidhi zawadi mjamzito,Samira Kassim mkono wa kushoto katika hospital ya rufaa Bombo mkoani Tanga
Pichani ni Meneja wa benki Azania Tawi la Tanga, Hajira Mmambe,mkono wa kulia,Akimkabidhi muuguzi wa zamu katika hospital ya rufaa Bombo mkoani hapo akieleza lengo ni sehemu ya kurudisha kile kilichopatika kutoka kwa wananchi.

Pichani ni wafanyakazi wa benki Azania Tawi la Tanga,wakiwa katika wodi tatu wakikabidhi zawadi katika wodi hospital ya rufaa Bombo mkoani hapo ambapo ni sehemu ya kurudisha kile kilichopatika kutoka kwa wananchi.

Pichani ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa kwenye picha ya pamoja na muuguzi wa zamu mara baada ya kukabidhi zawadi kwa wagonjwa 41 hospitali ya rufaa ya Bombo mkoni Tanga.

No comments:

Post a Comment