Sunday, 9 October 2022

UFUNFUNGUZI MASHIMNDANO YA SHIMIWI MWAKA 2022 ILIKUWA HIVI,,,

Pichani ni WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora,Jenister Mhagama  akifungua mashindano ya SHIMIWI mwaka 2022 huku akiwataka waajiri wa Wizara,Idara na wakala wa serikal kutenga bajeti ya kutosha ya kuwalipa mafungu ya mafunzo,likizo na michezo bila kuwakwamisha watumishi kujenga afya zao.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora,Jenister Mhagama  amewataka waajiri wa Wizara,Idara na wakala wa serikal kutenga bajeti kutosha ya kuwalipa mafungu ya mafunzo,likizo na michezo bila kuwakwamisha watumishi kujenga afya.

Waziri  Mhagama alitoa maagizo hayo jana wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kstika ufunguzi wa Mashindano ya Sgirikisho la Wizara na idara za Serikali (Shimiwi) yanayofanyika jijini Tanga.

Amesema lengo kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao ya kila siku bila kuwa na vikwazo vya kiutumishi ikiwamo kutofanya upendeleo wakati wa kuwapandisha madaraja.

Pia aliwataka waajiri kufuatilia kwa karibu mienendo ya watumishi ikiwamo tarehe walizoanzia utumishi ili wapande madaraja bila kuwachelewesha hasa ikizingatiwa kuwa katika bajeti ya mwaka 2022 -2023 Serikali imetenga mafungu.

Aidha,alibainisha kueleza kwamba kusimamia nidhamu na kanuni zilizopo za kiutumishi ili watumishi watekeleze majukumu yao kwa tija.

Akiwasilisha salaam za Waziri Mkuu alisema pia aliwaagiza waajiri kutenda haki katika kusimamia utendajikazi na wajiepushe na upendeleo wakati wa kukaimisha nafasi huku wakiondoa muhali kwa watumishi wao lakini watekeleze kikamilifu usimamiaji wa raslimali fedha.

Awali,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Omari Mgumba aliwataka watumishi kuitumia michezo hiyo kutangaza vivutio vya kitalii na uwekezaji vilivyopo Tanga ili kuwezesha kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuongeza uchumi.
Mwisho.



Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Omari Mgumba aakiangalia timu shiriki 63 akitumia nafasi hiyo kwa kuwataka watumishi kuitumia michezo hiyo kutangaza vivutio vya kitalii na uwekezaji vilivyopo Tanga ili kuwezesha kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuongeza uchumi.


 Pichani ni miongoni mwa timu shiriki katika mashindano ya SHIMIWI.

No comments:

Post a Comment