Sunday, 9 October 2022

KAMPUNI YA AGROCOM AFRIKA IMEJIPANGA KUTUMIA MASHINDANO YA SHIMIWI KUBORESHA MAISHA YA WATUMISHI NCHINI,,,

Pichani ni Afisa Masoko wa Kampuni Agricom Afrika, Baraka Konkara  akiwa uwanja wa soka Mkwakwani jijini Tanga,amesema Lengo la kuwa miongoni mwa wadhamini mashindano ya SHIMIWI Mwaka 2022 ni kuhamasisha watumishi kutumia fursa zilizopo ili kuweza kuboresha maisha yao kabla ya kustaafu.

     NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WADHAMINI wa Mashindano ya SHIMIWI, Kampuni ya Agrocom Afrika isiyo ya kiserikal imekuja na Program ya Mtumishi Shambani lengo likiwa kuwafikia Wafanyakazi kuwapatia elimu jinsi ya kuendesha Kilimo na kufikiwa na huduma za kiufundi.

Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Baraka Kontara akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga, ambako kunafanyika mashindano ya ShimIwi kwa Mwaka 2022 miongoni mwa wadhamini wakiwa Agrocom Afrika.

Katika mazungumzo yake hayo, Afisa Masoko huyo alisema, wafanyakazi  wa Serikali pia wanashiriki Kilimo na watakaponunua Vifaa ikiwemo mitambo kwa Kampuni hiyo watafikiwa kwa huduma za kiufundi mahali popote walipo.

Alisema kwamba, kabla ya kuwapatia vifaa hivyo Kampuni hiyo inawajibika kuwapatia elimu maopereta 'operators' waendesha mitambo ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku Agricom wakiwajibika kuihudumia.

Kwa mujibu wa afisa huyo, lengo la mpango huo ni kuondosha uwezekano wa vifaa hivyo vya Kilimo 'Mitambo' kuharibika mara kwa mra na huku ikiozea mashambani hivyo kupitia Kampeni ya Mtumishi Shambani hasa itapungua.

Alisema kwamba, wamechukua hatua hiyo baada ya Serikali ya awamu ya Sita  kuweka kipaumbele kwenye sekta ya Kilimo na baada ya Agricom kugushwa na kuona kuna haja ya wao  kutumia fursa hiyo kuwa miongoni mwa wadhamini kuja kuzungumza na Wafanyakazi.

" Wafanyakazi wa Serikali nao wana nafasi kubwa kuitumia fursa ya kilimo,na Serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele suala la Kilimo hivyo tukatumia fursa hii kama wadhamini kuja kuzungumza nao kupitia Mashindano haya ya ,Konkara .

Aidha,aliongeza kueleza kuwa,Mashindano hayo yamewapatia fursa ya kuzungumza lugha moja na wafanyakazi wa Serikali  na kwamba Kampuni imekuja na uzinduzi wa kampeni ya Mtumishi Shambani iliyozinduliwana Waziri Jenister Mhagama.

Mbali na Agricom Afrika kujipambanua kuwa inatoa  huduma za kiufundi lakini pia inatoa huduma ya mikopo kupitia taasisi za fedha ambazo mtumishi wa umma anaponunua atatumia muda mfupi kupata mikopo na kuweza kulipa.

Michezo ya Shimiwi kwa Mwaka 2022 inafanyika Mkoani Tanga ambapo madhumuni makuu ni kuboresha afya za Wafanyakazi, kujenga mahusiano kazini ikiwa ni pamoja na kujaribu kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishi hapa nchini.
Mwisho.

 

No comments:

Post a Comment