NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KAMPUNI ya
Agricom Afrika imesema ina mpango mkakati wa
kuwekeza kwa wakulima wa zao la mkonge nchini ili kuwawezesha kulima zao
hilo kwa tija na kuinua kipato na uchumi wao kwa kulima kisasa.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Baraka Konkara ambapo amesema kwamba
lengo la kuwekeza katika zao hilo ni kutoa fursa kwa wakulima wa mazao mbalimbali ili waweze
kunufaika na fursa zilizopo.
Alisema
tayari wameshajenga mahusiano mazuri baina yao na wakulima wa zao la mkonge ikiwemo Amcos mkoani Tanga lengo
likiwa ni kulima kilimo cha kisasa na kuwawezesha kunufaika na kilimo
“Kiukweli
kuna haja kubwa ya wakulima kuweza kubadilika kulima kisasa ,kuleta tija kupata
mavuno yenye kuleta mafanikio kwa mtumishi,hivyo ni muhimu kutumia zana za kisasa kutoka kwenye kilimo cha mazoea,”alisema Afisa masoko huyo Konkara huku akisistiza wakulima kujitokeza kunufaika na kampuni hiyo.
Konkara alibainisha kwamba lengo la kampuni
hiyo kuwekeza ni baada ya kuona ndani ya miaka mitatu zao hilo kuonesha kuleta
mabadailiko katika faida zake hapa
nchini.
Akizungumzia
zaidi afisa masoko huyo alisema kuwa tangu kuwekeza kwenye michezo jijini Tanga kujikita kutoa elimu kwa watumishi na jamii,tumeweza kuona mabadiliko na mwamko mkubwa kwa baadhi wananchi wa kada mbalimbali kujitokeza
kuhitaji huduma za
mikopo vifaa vya kilimo.
Hata hivyo,alisema kwamba lengo la kuweka kambi kuitumia michezo ya SHIMIWI ili
kuisaidia serikali ya Awamu ya sita kupitia sekta ya michezo na kilimo kutengeneza mazingira rahisi zaidi watumishi kujiongezea kipato kupitia shambani.
Pia alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kutengeneza mazingira mazuri kwa Wizara , idara na Taasisi za serikali ili waweze kukopa au kununua vitendea kazi ili kutimiza lengo la mtumishi Shambani.
Afisa masoko huyo, alizitaja miongoni mwa AMCOS ambazo tayari wameshafanya mazungumzo ili kuziwezesha kuwapata wakulima wa zao la Mkonge ni Magunga , Mwerya ,Magoma, Hale zilizopo Korogwe Mkoani Tanga.
Pia alibainisha kueleza kwamba tayari Agricom imefanikiwa kuketi na Bodi ya Mkonge Tanzania,lengo likiwa kuweka mazingira mazuri ya kuongeza tija kwa wakulima na kuwajengea uwezo kutimiza ndoto zao kupitia kilimo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment