WASAFIRISHAJI wa Bodaboda Jijini Tanga, wana mpango wa kutimiza ndoto zao kuboresha maisha baada ya Benki ya NMB kuonesha nia ya kuwapatia Mikopo nafuu ya Pikipiki na Bajaji ili kuondokana na changamoto ya mikataba.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Pikipiki na Bajaj (UWAPIBATA)Jijini Tanga, Mohamed Chande katika kikao cha mwaka cha kuwasilisha mapato na matumizi,ambapo aliomba ridhaa kufanya maboresho ya katiba.
Alisema,tayari wamefanya mikakati mbalimbali na wadau ikiwemo benki ya NMB lengo kuwawezesha waendesha bodaboda kupata mikopo na bima ili kuondokana na changamoto ya kukatiza mikataba na watu binafsi.
Chande alisema kuwa,Lengo la uongozi kufanya mazungumzo na NMB ni kutokana na changamoto zinazowakumba bodaboda ikiwemo kukopeshwa pikipiki na watu binafsi huku wakilazimika kulipa gharama mara mbili yake.
Alibainisha kwamba msafirishaji (bodaboda) hupewa pikipiki yenye thamani ya sh 2 million huku akitakiwa kulipa sh 4 million na wakati mwingine hushindwa kurejesha na kunyang'anywa vitendea kazi kwa kuvunja mkataba.
Pamoja na hayo Katibu huyo alisema,kwamba bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya wanachama wake kuwa wazito katika ulipaji ada ili kuwezesha kuwasaidia pindi wanapopata majanga barabarani.
Mwenyekiti,Chande alisema kuwa wameendelea kuwaelimisha wanachama wao kuona umuhimu wa kuchangia kwa vile fedha hizo zimekuwa zikisaidia shughuli za uendeshaji chama.
Mbali na uendeshaji chama lakini pia fedha hizo zimekuwa zikiwasaidia pindi wanapofikwa na majanga mbalimbali kama vile ajali.
Zuberi Juma ambaye ni bodaboda alisema, mpango wa NMB wanaokuja nao katika kuwakopesha utawasaidia kujikwamua kiuchumi huku wakiwa na uhakika wa kumiliki vyombo vyao.
Juma alisema, benki hiyo itakapowakopesha watakuwa wakilipa mikopo yao kwa utaratibu mzuri sanjari na kujiwekea akiba tofauti na ilivyo sasa.
Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani,Koplo Hamis alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wasafirishaji hao kusajili vyombo vyao ili kusaidia kudhibiti vitendo vya uhalifu.
Sambamba na hilo aliwataka kushikamana na kuhakikisha wanajiwekea akiba kwa kujianzishia vyanzo mbadala ikiwemo mfuko wa waendesha bodaboda wilayani Tanga.
Mwisho.
Amesema kwamba muda umefika dafutari hilo la Usajili la namba mpya ambalo liko kwa mlezi wa chama hicho cha waendesha bodaboda UWAPIBATA ambaye ni mkuu wa kitengo cha usalama barabarani ''RTO'' kuna haja ya kurejesha kwenye chama ili kuondoa idadi kubwa ya namba ambapo mpaka sasa imefika elfu moja huku bajaji zikiwa ni chache.
Pichani ni miongoni mwa wanachama wa Chama cha waendesha bodaboda wa Pikipiki na Bajaji wakiwasikiliza viongozi mbalimbali katika kikao cha mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment