Pichani ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Suleiman Mzee Suleiman akizungumza na habari wa habari mkoani hapo (hawapo pichani),akiwasa wagombea kuzingatia maadili kuelekea uchaguzi ngazi ya mkoa.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA.
WAKATI Chama Cha Mapinduzi CCM kikielekea kwenye uchaguzi wake wa ngazi ya mkoa huo,kimetoa onyo kwa Wanachama wenye nia ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi,kuzingatia maadili huku wakiepuka kujiingiza kwenye udalali wa kisiasa kwa maana ya kupanga safu.
Onyo hilo limetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Suleiman Mzee Suleiman wakati akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani),amewasa tabia za baadhi ya watu kutozingatia maadili kuelekea uchaguzi ndani.
Suleiman ambaye ni Msiamamizi Mkuu wa Uchaguzi Mkoani Tanga, alisema kwa wale watakaokosa kuzingatia maadili ya chama hicho wasije wakajishangaa kujikuta wako hatarini ambapo hatua za kinidhamu hazitasita kuchukuliwa dhidi ya wanaokiuka taratibu zilizopo ndani ya CCM.
"Tunaelekea kwenye uchaguzi wa ngazi ya mkoa wagombea wanatakiwa kuwa watulivu kufuata taratibu zilizopo,ili waweze kuwa na sifa ndani ya CCM, mkurugenzi mkuu wa uchaguzi kubwa ni kusimamia maadili,tunahitaji viongozi bora na sio bora kiongozi"alisema.
Aidha Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Tanga,alisema kwamba kila mwanachama ambaye amefuata taratibu zilizopo,na sheria za uchaguzi zitazingatiwa ili kuweza kuwapata viongozi bora.
Aidha,alibainisha kueleza kwamba kiongozi bora ni yule ambaye hana tabia ya kujipitishapitisha wala kujitangaza kwa wanachama na kwamba wanachama wote chama chao kinawafahamu huku akieleza kuwa mtandao umetengenezwa kufuatilia mienendo na tabia za wanachama wake.
"Tutakapogundua ajijue yule aliyempanga mtu ama aliyejipitisha mapema ajue jina lake halitarudi katika kugombea nafasi za uongozi,uongozi wa CCM unadumu ndani ya miaka mitano"alisema Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman.
Katibu huyo wa CCM Mkoa waa Tanga,Pia alisema kuwa kwa wale waliopo kwenye madaraka na kutumia nafasi zao vibaya watakuwa wamejenga mapambano na kanuni za maadili ya Chama Cha Mapinduzi ambacho hakitaweza kuwa tayari kumvumilia.
Kwa mujibu wa Msimamizi huyo wa uchaguzi wa CCM Mkoani Tanga,alisema kwamba lengo la chama hicho ni kuweza kupata viongozi ambao watakaoweza kukivusha Chama hicho katika kuweza kuwahudumia vyema Watanzania walio wengi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment