NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TAASISI ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga ,katika uchunguzi imefanikiwa kubaini jumla wa wagonjwa hewa 313 wa VVU Kwenye mfumo wa Usajili wa wagonjwa hao wilayani Muheza kwa lengo ili kuonyesha takwimu ziko juu ili kujinufaisha.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga ,Zainabu Bakari wakati akitoa taarifa hiyo ofisini kwake wakati akizungumza na waandashi wa habari jijini Tanga.
Akisoma taarifa yake ya kipindi cha julai hadi September mwaka huu,alisema kwamba awali TAKUKURU ilipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kwamba kuna baadhi ya watoa huduma idara za afya wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kufanya udanganyifu wa kusajili watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi VVU kinyume na utaratibu.
Alisema kuwa watoa huduma hao walikuwa wakiingiza majina hewa ya wagonjwa ili kuonyesha kuwa twakimuza za wanaoishi na VVU kuonekana ziko juu kwa maslahi yao binafsi huku ikiwa ni kosa kisheria.
Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani Tanga,Zainabu alisema baada yakupokea na kufuatilia baadhi ya Zahanati wilayani Muheza,kuanza utekelezaji wa majukumu yao na kufanikiwa kubaini kuna wagonjwa 313 ambao siyo halisi kwa upatikanaji wake.
''Takukutu baada ya kupata taarifa kufuatilia wahudumu wa afya wanaohusika na zoezi la kuwasajili na kuwafuatilia wagonjwa wanaoishi na VVU,pia tumebaini wamekuwa wakilipwa posho ya gharama ya usafiri shilingi 20,000 kwa siku kila wanapotoka kwenda kuwatembelea wagonjwa''Alisema Zainabu.
Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani Tanga,Zainabu alibaisha kueleza kuwa fedha hizo zilikuwa zikilipwa na Shirika la afya AMREF kwa ajili ya kazi ya kufuatilia kila mgonjwa lengo likiwa kuhakikisha hali zao za kiafya zinaimarika.
Alieleza baada ya kufuatilia na kujiridhisha iliitisha kikao ca pamoja kilichohusisha ofisi ya mganga mkuu wilayani Muheza na wanaohusika kuhudumia watu wanaoishi na VVU pamoja na AMREF.
Akifafanua zaidi sababu zilizopelekea kwa watumishi hao kutokuwa waadilifu ni kutumiwa pesa moja kwa moja kwa mhudumu kupitia simu yake ya mkononi na kwa kuweka takwimu hewa kwa lengo la kujiongezea posho.
Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoani Tanga,alieleza kwamba baada hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuitisha kiako cha pamoja kati ya Takukuru na ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Muhuza (DMO) na watendaji wake wote wanaohusika na kuhudumia watu wanaoishi na VVU pamoja na Amref.
Hata hivyo, alisema katika kikao hicho Takukuru iwasilisha yaliyobainika katika ukaguzi kwa kuwatembelea jumla ya zahati 7 katika 16 zilizopo wailayani Muheza na kubaini kuwepo kwa tatizo hilo, ambapo ilimuagiza Mganga mkuu wa Wilaya hiyo kufanya uhakiki wa Takwimuza wagonjwa wote wanaoishi na VVU na kutoa taarifa za uhakiki.
“Baada ya agizo hilo , ilibainika kuwepo kwa jumla ya wagonjwa hewa 313, ambapo idadi hiyo ya wagonjwa hewa iliondolewa, na kupewa barua za kujieleza kwa kitendo caho cha kusajiuli wagonjwa hewa , lakini wizara ya Afya imetoa maelekezo ya kufanyika uhakiki kwa wateja wanaotumia dawa ambazo sio halisi.”alifafanua Bi Zainabu.
Hata hivyo,TAKUKURU Mkoa wa Tanga imetumia nafasi hiyo kuwasihi watumishi wa umma kufanya kazi kwa kwa mujibu wa kanuni , taratibu , sheria na miongozo iliyopo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment