Pichani ni Wakili wa Serikali wa Jeshi la Uhamiaji,Moses Yogo akiwa nje ya Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tanga,akizungumza na waandishi wa habari ''hawapo pichani''mara baada ya kuwasomea washtakiwa 75 shtaka
lao.
lao.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Mkoani Tanga imewahukumu Waethiopia 75 kila mmoja kutumikia Kifungo cha Mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Shilingi 500,000 baada ya kukiri kosa la kuingia nchini kinyume na taratibu.
Katika kesi hiyo namba 94 ya mwaka 2022 Mahakama ya Hakimu mkazi,Simon Kobero mbele ya,wakili wa serikali Idara ya Uhamiaji,Moses Yogo akiwasomea shtaka lao
wahamiaji hao haramu alieleza wote kwa pamoja walifanya kosa hilo huko wilayani Handeni mkoani Tanga.
Baada ya watuhumiwa kusomewa mashtaka hayo, kupitia mkalimani wao, walikiri kutenda kosa hilo la kuingia nchini kinyume na taratibu za kisheria kifungu no.45 1(i) na 2ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2016.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Kobero aliwahukumu kila mmoja kwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini kiasi cha Shilingi Laki tano (500,000/=).
Hata hivyo washtakiwa hao wote hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kulipa faini hiyo iliyotolewa na Mahakama, hivyo wamekwenda jela kutumikia kifungo hicho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment