Pichani ni ambaye ameshika karatasi ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga SACP,Henry Mwaibambe akisoma taarifa ya matukio mawili kwa waandishi wa habari likiwemo la Marehemu Defao Mkulima na mkazi wa Miembeni wilayani Muheza.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
ASKARI wa Jeshi la akiba Mgambo,Samson Stephen (25) anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi Athumani Ramadhani maarufu 'Defao'.
Askari Mgambo huyo wa Magoroto Estate anadaiwa kumuu Athuman 'Defao' kwa kumpiga risasi akitumia bunduki aina ya Shortgun.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga SACP,Henry Mwaibambe akisoma taarifa yake kwa waandishi wa habari alisema kuwa Marehemu Defao alikuwa Mkulima na mkazi wa Miembeni wilayani Muheza.
Alisema kwamba, chanzo cha tukio hilo ni Marehemu Athumani Defao kuingia kwenye Msitu mali ya Amboni Ltd kwa lengo la kukata miti ya nguzo za nyumba.
Kamanda Mwaibambe alibainisha kueleza kuwa, katika purukushani za kukamatwa inadaiwa Marehemu alitaka kumkata Panga Samson (Mlinzi).
Hata hivyo,Mtuhumiwa huyo baada ya mauaji hayo alijisalimisha mwenyewe kwa Jeshi la Polisi baada ya tukio hilo la mauaji.
Wakati huo huo,Jeshi la polisi mkoani Tanga linamshikilia,Fredy Kakiko (67) ambaye ni mmiliki wa Ukumbi wa BMK Sahare akidaiwa kuhusika na uhalifu uliotokea maeneo tofauti likiwemo la Jiji la Tanga na Dar es Salaam.
Mwisho.
.
.
No comments:
Post a Comment