Wednesday, 16 November 2022

POLISI TANGA,YASHIKILIA PIKIPIKI 20 ZILIZOKUWA ZIKITUMIKA KWENYE MATUKIO YA UHALIFU,,,,

Pichani ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,SACP Henry Mwaibambe akizungumzia Operesheni iliyofanikisha kusalimishwa silaha 488.

 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

OPERESHENI iliyofanywa na jeshi la polisi mkoani Tanga,limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali kusalimishwa miongoni mwake yakiwemo Magobore 457, bunduki aina ya Shortgun 25, Rifle 3 na bastola 3 hivyo kufanya jumla yake kuwa 488.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,SACP Henry Mwaibambe alisema ni miongoni mwa utekeleza kazi na agizo la kusalimisha silaha.

Alisema, silaha hizo zimepatikana wakati wa zoezi la Usalimishaji huku akitanabaisha kuwa Polisi imeendelea na Operesheni zake ili kuimarisha hali ya Ulinzi na Usalama.

Alisema, katika operesheni hizo, pia wamefanikiwa kukamata Pikipiki 20 zilizokuwa zikitumika kwenye matukio mbalimbali ya Uhalifu Mkoani humo.

Alisema, miongoni mwa Pikipiki hizo tatu zinahusishwa na matukio ya Wizi wa mifugo huku watuhumiwa wake wakishikiliwa, Pikipiki 12 zinahusishwa kwa matukio ya unyang'anyi,uporaji simu na mikoba na watuhumiwa 7 wamekamatwa.

Pia Pikipiki tatu zinahusishwa na matukio ya Usafirishaji wa dawa za kulevya na wahamiaji haramu wakati pikipiki nyingine 2 zinahusishwa na watu waliotaka kuvunja na kuiba.

Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga alisema watuhumiwa waliokamatwa watafikishwa Mahakamani mara taratibu zitakapokamilika.

Mbali na kuzungumzia matukio hayo, pia alisema tarehe 3/10/2022 huko Kisosora alikamatwa Huruma Josephat akiwa na Silaha inayodhaniwa kuwa bandia aina ya Pistor.

Ameeleza kuwa silaha hiyo alikuwa ameihifadhi kwenye begi lake la mgongoni na kwamba upelelezi unaendelea huku mtandao wa mtuhumiwa huo ukisakwa ili hatua za kisheria kuchukuliwa.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment