Wednesday, 16 November 2022

JESHI LA UHAMIAJI TANGA,,LAELEZA SAKATA LA KUWAKAMATA RAIA WAETHIOPIA 75,DEREVA NA UTINGO WALIVYOTELEKEZA LORI,,,

 Pichani ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoani Tanga,Kagimbo Hosea akiwa ofisini kwake akizungumzia sakata la kukamatwa kwa raia wa Ethiopia 75 kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume na utaratibu.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
 Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Uhamiaji Mkoani Tanga,Kagimbo Hosea akiwa ofisini kwake akielezea tukio la kukamatwa kwa raia wa Ethiopia 75 kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume na utaratibu.

Alisema kwamba raia hao walikamatwa juzi saa 3.30 alaasiri huko katika kijiji cha Kitumbi tarafa ya Mazingara kilichopo wilayani Handeni. 

Kamishna msaidizi Kagimbo alisema walikutwa kwenye Lori lenye namba za usajili KBR 911 Z,Tela ZD 2426  gari hhilo lililokamatwa ni mali ya Kampuni ya WARTA Enterprises  ya Mombasa nchini Kenya.

Aidha,alibainisha kuwa Waethiopia hao wamekamatwa kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume na sheria ya uhamiaji kifungu 45 (1) (i) sura ya 59 iliyofanyiwa marekebisho 2016.

Alisema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo la ukaguzi wa gari ndipo dereva na utingo wakitelekeza Lori hilo pembeni mwa barabara ya Mkata-Segera likiwa na Wahamiaji hao ambao ni raia wa Waethiopia.

Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonesha gari hilo liliingia nchini Tanzania kupitia mpaka wa Tarakea Mkoani Kilimanjaro mnamo tarehe 19/10/2022 ambapo lilitakiwa kuondoka 18/12/2022.

Alisema Gari hilo linashikiliwa na katika upekuzi zilikutwa  nyaraka za raia wawili wa Kenya ambao ni Emmanuel Kirui na Gladys Cherop. Uchunguzi unaendelea kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment