Sunday, 20 November 2022

Pichani ni Kocha wa Timu ya Tanesco,Juma Sungura akiwa katika uwanja wa shule ya msingi Sahare jijini mara baada ya mchezo wao,dhidi DUCE amesema katika michuano ya SHIMUTA wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika michezo ambayo wanashiriki.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TIMU ya nishati ya umeme Tanesco imesema mwaka huu imedhamiria kurudisha ari ya michezo mbalimbali ukiwemo wa soka ambao ulipoteza ramani tangu mwaka 2019 walipoibuka kuwa mabingwa mkoani mwanza.

Hata hivyo, imesema lengo la timu hiyo ya shirika hilo la Tanesco ni kuhakikisha kila mchezo kusaka ponti 3,ambazo ni muhimu sana katika michuano hiyo ili kuweza kusonga mbele.

Kocha Sungura ametoa matambo hayo katika Viwanja mbalimbali Jijini Tanga mara baada ya mchezo wao dhidi ya DUCE ambapo waliibuka kwa ushindi wa goli 1-0.

Kocha wa Timu ya DUCE, Jackob Ngogo amesema kushindwa kwao katika mechi hiyo ni sehemu ya mchezo baada ya mabeki wake kushindwa kujipanga vyema.

Aidha alikiri udhaifu kwa kupoteza mchezo wake wa awali dhidi ya BOT kwa kufungwa mabao 2-0 akisema wanajipanga kwa mechi zijazo.

"Tangu tulipo chukua ubingwa Mwanza tulipotea kwenye ramani ya sasa mwaka huu tumedhamiria,mashindano ya SHIMUTA mwaka huu tumejipanga' " alisema Kocha wa Tanesco Sungura.

Kocha wa Tanesco,Sungura pia ameelezea faraja yake ya mwenendo wa michezo ambayo wamefanya vizuri katika mashindano hayo,na kuwataka mashabiki waendelee kuwaamini na kutoa sapoti ili kuweza kufikia malengo yao.

Pia amebainisha kueleza kwamba mechi ni ngumu kutokana na kila timu imejiandaa lakini tutahakikisha tunatimiza malengo yetu,kuibuka bingwa.
Mwisho.

Pichani ni timu ya Tanesco inayoshiriki michuano ya SHIMUTA.

 

No comments:

Post a Comment