Pichani mkono wa kulia mwanaume ni Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa waTanga,Victor Swella akiwasilisha taarifa yake kwa waandishi wa habari Jijini Tanga katika kutimiza majukumu yao ya ufuatiliaji miradi mbalimbali ya maendeleo.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TAASISI ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tanga, imefanikiwa kudhibiti fedha sh. 17,000,000,00 million kwenye miradi ya madarasa iliyopata fedha kutoka serikalini.
Hata hivyo,imesema Serikal ingepata hasara kutokana na ukiukwaji mwongozo wa matumizi ya fedha kupitia 'Force' Akaunti na hivyo kufanikiwa kuokoa fedha za Umma kwenye utekelezaji miradi ya Maendeleo.
Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa waTanga, Victor Swella ametoa taarifa hiyo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga ambapo alisema fedha hizo zimenusurika kutokana na ufuatiliaji.
Swella alisema,lengo ni serikal kuepuka kupata sababu ya ukiukwaji wa taratibu katika manunuzi ya bidhaa mbalimbali za ujenzi wa miradi husika ya madarasa mkoani hapo.

Alisema kwamba kipindi cha Oktoba na Disemba 2022, Takukuru imetekeleza majukumu kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi kwenye miradi ya maendeleo hasa ile itokanayo na fedha za Serikali kuu.
Aliitaja, miradi iliyofuatiliwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari ambapo wilayani Korogwe Shule za Semkiwa Sekondari, Joel Bendera na Chief Kimweri.
Swella alisema kuwa fedha zilizotengwa na Serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiuo ya ujenzi eneo hilo ni sh 200 milioni.
Hata hivyo,Takukuru ilibaini kwamba wakuu wa shule na wasimamizi waliingilia mwongozo na mchakato wa manunuzi hatua ambayo ingesababisha gharama za uendeshaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa 11 katika shule za sekondari Nyerere,Kimweri na Semkiwa kupanda kufikia sh 237 milioni hivyo ujenzi kushindwa kukamilika kama ilivyopangwa.
Katika ufuatiliaji wa Takukuru, uongozi wa shule, mamlaka husika na kamati matokeo yake uwazi ukaongezeka,hujuma na upendeleo vikatoweka.
Kaimu huyo mkuu wa Takukuru alisema kwa hali hiyo miradi yote mitatu ilikamilika kwa wakati na kwamba ufuatiliaji usingefanyika sh 17 million zingepotea na serikali kupata hasara.
Katika hatua nyingine Takukuru imefanikiwa kufanya kazi ya ufuatiliaji miradi 95 ya maendeleo yenye thamani zaidi ya sh 12 bilioni mkoani Tanga.
Alisema miongoni mwa miradi hiyo 69 ni ujenzi wa vyumba vya madarasa 137 kwa zaidi ya sh 200 bilioni ikifahamika kama miradi ya pochi la mama fedha kutoka serikali kuu.
Mwisho.

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa waTanga, Victor Swella akiwa na miongoni mwa maafisa wa ofisi hiyo mkoani hapo.
No comments:
Post a Comment