Thursday, 9 March 2023

WANANCHI WA MTAA WA KWANJEKA A,WAMEANDAA MAULID KUFANYA UZINDUZI WA KISIMA KILICHO JENGA KUPITIA MPANGO WA TASAF,,,,,

Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni Diwani wa kata ya Mnyanjani,Simba Kayaga akiwahutubia wananchi wa mtaa wa Kwanjeka A akiwataka kuwa walinzi wa mradi wa kisima ili uweze kupata huduma hiyo jirani hata kipindi cha kiangazi.

NA SOPHIA WAKATI, TANGA.
DIWANI wa Kata ya Mnyanjani,Simba Kayaga,amewataka wananchi wa Mtaa wa Kwanjeka 'A' kutunza na kutumia vizuri mradi wa Kisima cha Maji uliojengwa kwa ufadhili wa TASAF.

Kayaga alitoa rai hiyo juzi kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Kisima hicho alisema kujengwa kwa mradi huo imekuwa ukombozi kwa wananchi walio wengi.

Alisema kuwa,ni vyema mradi huo ukatunzwa huku ukitumika kwa kusudio tarajiwa lengo likiwa kuwezesha Kisima hicho kutumika kwa jamii iliyopo wakati huu na ule ujao.

Kwa upande waka,Afisa Mtendaji mtaa wa Kwanjeka A, Samira Msumari alitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kuwezesha upatikanaji wa fedha kupitia TASAF kufanikisha mradi huo kwa kisima kwa jamii.

Samira alisema kwamba, mbali na mradi huo kuibuliwa na walengwa wa mpango wa TASAF lakini bado utanufaisha wananchi wote wanaoishi kwenye mtaa wa Kwanjeka 'A'.

Amewapongeza walengwa wa mpango huo kwa hamasa waliounyesha wakati wa utekelezaji mradi ambao ni utaratibu mpya wa ajira za muda kupitia mpango wa TASAF.

Nae Msimamizi uchimbaji wa kisima hicho,John Magome aliwaasa wananchi kwa kuwaeleza kuwa kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake katika kutunza miundombinu hiyo.

Pia ametumia nafasi hiyo kuwashauri wananchi matumizi mazuri ya Kisima hicho ikiwa ni kuenzi juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anayefanya kazi kubwa kutafuta fedha za kutekeleza miradi hapa nchini.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwemo walengwa wa mpango wa TASAF,Mwanaidi Ally na Mwanahamis Ramadhan walishukuru kujengwa Kisima hicho huku wakiomba kutosahauliwa katika mipango mingine ya maendeleo.

Mwanaidi alisema kuwa mradi huo utakuwa suluhisho kwa kina mama awali awali walikuwa wakitumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji safi na salama.
Mwisho.



Pichani ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kwanjeka A,katika hafla ya uzinduzi wa kisima akiwashukuru viongozi wa TASAF halmashauri ya jiji la Tanga,kuwezesha kupata mradi huo ambao utakuwa mkombozi kwa wananchi wake.

Picha ni Afisa Mtendaji mtaa wa Kwanjeka A, Samira Msumari akitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kuwezesha upatikanaji wa fedha kupitia TASAF na wananchi kutoa ushirikiano kukamilika kwa wakati.


Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni Msimamizi uchimbaji wa kisima hicho,John Magome ambapo alitumia nafasi hiyo akiwaeleza wananchi kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake katika kutunza miundombinu hiyo.

Pichani mkono wa kulia ni Diwani wa kata ya Mnyanjani,Simba Kayaga akimtwika ndoo ya maji kichwani mkazi wa mtaa wa Kwanjeka A,katika hafla ya uzinduzi wa kisima alipokuwa mgeni rasmi.

Kisima kilichojengwa na wanufaika kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kupitia mpango wa TASAF

Pichani ni baadhi ya wananchi wakifuatilia maulidi hafla ya uzinduzi wa kisima,

Miongoni mwa wananchi wa Kwanjeka A,wakiwasikiliza viongozi mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa kisima.

Picha ni viongozi mbalimbali wakifuatilia Maulid katika hafla ya uzinduzi wa kisima kilichojengwa kupitia mpango wa TASAF.,
 

No comments:

Post a Comment