NA SOPHIA WAKATI, TANGA
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, limeidhinisha Bajeti ya sh 72,111,627,000 katika Mwaka wa fedha 2023/2024.
Meya wa Jiji la Tanga,Abrahaman Shiloo amesema kwamba, bajeti hiyo ni ile itakayokidhi maisha na matarajio ya Watu wa Tanga.
Katika kikao hicho cha bajeti, Meya Shiloo alisema kuwa, bajeti hiyo ni bora kuliko zilizopita kwa vile ina maridhiano makubwa ya madiwani wote.
Aidha alisema weledi na umahiri wa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga na wasaidizi wake umewezesha kupatikana kwa bajeti hiyo bora.
Kwa mujibu wa Meya Shiloo, alisema kuwa mchanganuo huo wa bajeti sh 40,605,222,000 Bilioni ikiwa ni Mishahara ya Wafanyakazi ili waweze kufanyakazi kwa tija.
Shilingi sh 794,523,000 ni matumizi mengineyo kutoka Serikali pamoja na Mishahara na zaidi ya bilioni 4 ikiwa ni fedha kutoka kwa Wahisani.
Nyingine ni zaidi ya Bil 7 fedha za miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu na zaidi ya sh 19 bilioni zitakusanywa kupitia mapato ya ndani, mapato lindwa zaidi ya bilioni 5 na mapato yasiyolindwa zaidi ya bilioni 13.
Akizungumza katika kikao hicho cha baraza la madiwani, Mwenyekiti wa CCM wilaya wa TangaMeja Mstaafu Hamis Mkoba amewata watumishi,madiwani kuwa na umoja na mshikamano lengo kuwezesha mambo mengi mazuri katika Jiji la Tanga.
Pamoja na hayo alielezea wasiwasi wake juu ya mahusiano hayo kulegalega na kutanabaisha kwamba hali ikiendelea kuwa hivyo hata bajeti iliyopangwa itakuwa haina maana.
"Mahusiano yetu yameanza kulegalega, na yakiwa hivyo hata bajeti iliyoletwa itakuwa haina maana yoyote kwa wananchi wa jiji la Tanga"alisema Meja huyo Mstaafu Mkoba
Mwenyekiti huyo wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya,Mkoba pia amesema katika majukumu yao kinachosimamia utekelezwaji ni Ilani ya CCM na kuwataka wataalamu waliopo katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kuwa kitu kimoja ili kuweza kuwatumikia wananchi.
Mwisho.

Pichani ni miongoni mwa madiwani wa halmashauri ya jiji la Tanga,wakiteta jambo,baada ya kuidhinisha Bajeti ya sh 72,111,627,000 katika Mwaka wa fedha 2023-2024
Pichani ni miongoni mwa watumishi wa halmashauri ya jiji la Tanga,wakifuatilia kikao cha baraza la bajeti.,,
No comments:
Post a Comment