Thursday, 16 March 2023

JESHI LA UHAMIAJI MKOANI TANGA LILIVYOFANIKIWA KUWASHIKILIA WACHEZAJI NYUMBA ZA KULALA WAGENI KUTOKA CAMEROON KUFANYA MAZOEZI KWENYE TIMU ZA TANZANIA, KINYUME NA SHERIA,,,,

Pichani ni Kamanda wa jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Tanga,Hosea Kagimbo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake (hawapo pichani) mara baada ya kuwakamata wachezaji wa soka wahamiaji katika nyumba za kulala wageni New Maylodge na New  Palmlive barabara ya 4 na 20.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

Wachezaji wanne wa Cameroon wanaodaiwa kuja kwa ajili ya kupata mazoezi ya Usajili kwa timu za African Sports na Coastal, wanashikiliwa na Jeshi la Uhamiaji Mkoani Tanga kwa kuingia nchini hapa kinyume na taratibu za sheria.

 

Kamanda wa jeshi la Uhamiaji Mkoani Tanga,Kagimbo Hosea katika taarifa yake alisema kuwa, wahamiaji hao walikamatwa mnamo Machi 10 mwaka huu wakiwa katika nyumba za kulala wageni NewMaylodge na New  Palmlive barabara ya 4 na 20.

 

Alisema kwamba, katika uchunguzi wa awali unaonesha kuwa raia hao wa Cameroon waliingia nchini kupitia Uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere International Airport (JKNIA) na kupata Visa za matembezi za siku 90.

 

Alisema, wageni hao walionekana kupata Visa hizo za matembezi (HV) badala ya kupata zile za biashara (BV) kulingana na shughuli walizokuwa wakija kuzifanya akisema kuwa walikuja kwa msaada wa Wakala wao wa Michezo.

 

Afisa huyo wa uhamiaji Mkoa wa Tanga alimtaja Wakala wa Wahamiaji hao raia wa Cameroon kuwa anafahamika kwa jina la Benard Ntomondo Mfaume anayeishi Dar es Salaam akitanabaisha uchunguzi wa suala hilo kufanyika.

 

Alisema, katika uchunguzi uliofanyika kwa timu ya Coastal Union kupitia kwa Katibu wao wa Klabu ameeleza kutowatambua wala kuwafahamu huku akikosa kuwa na mawasiliano nao na kwamba barua za mwaliko walizonazo siyo sahihi.

 

Aidha Klabu ya African Sports wao wameeleza kutowata mbua wageni hao huku wakieleza kuwa wanayo barua ya Fountain Gate na Pamba Football Club huku akisistiza kusema kuwa bado Wakala wa Wacameroon hao anatafutwa.

 

Majina ya wahamiaji hao ni Romanus Gwa PPT No:AA253951 v/u 30/06/2027 HV v/u 21/04/2023 CN:991094176073, CedricDonard Pouangue Tchchoua PPT No:AA390933v/u 22/12/2027 HV v/u 05/04/2023 CN:991094127460.

 

Wengine ni Saisburunde Nji PPT No:1239847 v/u 22/09/2025 V/u 05/04/2023 CN:991094127473 na Rowand Benard Messi Atangana PPT No:AA389406 v/u 21/12/2027 HV v/u 21/04/2023  CN:9.

Mwisho.


Pichani ni Wachezaji wanne wa Cameroon wanaodaiwa kuja kwa ajili ya kufanya mazoezi ya Usajili kwa timu za African Sports na Coastal, wakiwa ofisi za Jeshi la Uhamiaji Mkoani Tanga kosa la kuingia nchini hapa kinyume na taratibu za sheria.

 


No comments:

Post a Comment