Friday, 17 March 2023

RC TANGA,,KINDAMBA ALIVYOWATAKA WAJUMBE WA CWT TANZANIA WENYE DHAMIRA YA KUANZISHA VURUGU wAVUNJE,KAMATI YA ULINZI IKO IMARA,,,

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba leo akiwaeleza wajumbe kuzingatia kanuni za uchaguzi zilizopo na kamati ya ulinzi na usalama iko imara wakati akifungua mkutano mkuu maalumu wa chama cha walimu Tanzania CWT uliofanyika jijini Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba amewataka wajumbe wa mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Walimu CWT nchini, kufanyika uchaguzi katika msingi wa Amani huku akiwaasa, kama kuna mtu amepanga kuanzisha Vurugu avunje dhamira yake hiyo kwa vile kamati ya Ulinzi na Usalama imeimarishwa.

Kindamba ametoa kauli hiyo (leo) alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo, ambapo amesema uchaguzi utafanyika kwa nafasi mbili tu ambazo hazijawekewa zuio la Mahakama.

Alisema kwamba, alishawasiliana na Rais wa CWT  Bi. Leya Ulaya aliyemtaarifu kuhusu zuio hilo la Mahakama hivyo hakuna budi kwa Wajumbe kufuata utawala wa sheria uliopo.

"Wakati inaandaliwa speech nilimuuliza Rais wa CWT position ikoje akasema kuna zuio la Mahakama,hivyo nafasi mbili zenye zuio hatutagusa tutatembea na nafasi ambazo hazijaguswa na mahakama" alisema Kindamba.

Aliongeza kusema kuwa nchi ya Tanzania inaongozwa kwa utawala wa sheria hivyo ni vyema watu wakakubaliana pasipo kudharau.

"Kama kulikuwa na joto linataka kupanda naomba ndugu zangu tulizeni roho zenu, nafasi mbili zenye court injuction hatutazigusa"alisema mkuu huyo wa mkoa wa Tanga,Kindamba.

Pia Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga alieleza kupokea taarifa juu ya watu kutaka kuanzisha vurugu ambapo alitumia jukwaa hilo kusisitiza uwepo wa amani akiwaeleza walimu kuwa wao ni watu waungwana na wastaarabu huku akiwatoa wasiwasi kwa kuwaambia ulinzi na usalama umeimarishwa ili mkutano kufanyika kwa amani.

"Wanaodhani kuna watu wanatania wasijaribu, sumu haionjwi, tufanye lile lililotuleta tumalize turejee vituo vyetu vya kazi"alisema Kindamba.

Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga,pia amewaasa walimu  hao kuhusu suala la kuwapata viongozi wao akiwataka kuchagua wale wenye uwezo wa kuongoza badala ya kufuata ushawishi wa watu au vikundi fulani.

Kindamba alibainisha kuleza kwamba, sababu kubwa ya kufanya uchaguzi kuwa nyeti ni kwa vile wale wanaochaguliwa wanabeba dhamana nzima ya taasisi husika.
Mwisho.

Pichani ni Katibu Mkuu wa chama cha walimu sekta binafsi Ruanda,Nkotanyi Faustin,amesema amefika kwenye mkutano huo kwa mshikamano uliopo miongoni mwao huku akiwaasa wajumbe kutochagua viongozi wa chama hicho kwa misingi ya rushwa.

Pia amesema kwamba kupitia mkutano huo iko haja kwa vipengele kadhaa kwenye katiba kufanyiwa marekebisho ili kuweza kuleta tija kwa viongozi na wanachama wa chama hicho.

Alisema kuna mambo hayahitajiki kufikishwa Mahakamani ila chama cha walimu kinapaswa kushughulika nayo kwa lengo la kuimarisha utendaji wao.

Mwisho.


Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu CWT Dodoma jiji, Prospar Mutungi amesema, ana matumaini makubwa kwa uchaguzi wa CWT Taifa kuwa shwari licha ya kujitokeza kwa sintofahamu kadhaa kwa baadhi ya watu kutaka kututengenezea visingizio vya vurugu ambazo zimeweza kutulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba.

Alisema kwamba amewasili jana (16/03/2023) kulikuwa na sintofahamu juu ya wajumbe kutishwa lakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga amewahakikishia amani na usalama kutawala mkutano huo.

Nafasi ambazo zinawaniwa kwenye uchaguzi huo ni ile ya Makamu wa Rais wa CWT na Katibu Mkuu huku nyingine zikiwa na zuio la Mahakama.

Miongoni mwa wajumbe wakimfuatilia Mkuu wa mkoa wa Tanga,akifungua mkutano huo.


 Miongoni mwa wajumbe wakimfuatilia Mkuu wa mkoa wa Tanga,akifungua mkutano huo.


Pichani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu CWT wilaya ya Ngara, Allen Deogratius amekiri ni kweli awali kuna vitu vilitaka kuibuka na kuleta sintofaham lakini baada ya mkuu wa mkoa wa Tanga,ana matumaini makubwa kwa uchaguzi wa CWT Taifa kuwa swari.

No comments:

Post a Comment