Saturday, 18 March 2023

RC TANGA,KINDAMBA AMESEMA UJIO WA MELI KUBWA KUTIA NANGA BANDARI YA TANGA ITAFUNGUA FURSA YA AJIRA,UCHUMI KUONGEZA KIPATO...




Pichani mkono wa kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba akizungumza na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga akieleza serikal inayoongonzwa na rais Dk.Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi Billion 272 kufanya maboresho,huku akiwataka kutanguliza uzalendo katika kutimiza majukumu yao ili kuwa kivutio kwa wafanyabiashara kupitisha mizigo na mkono wa kushoto ni meneja wa Bandari ya Tanga,Masoud Mrisha.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba, amewataka Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga kufanya kazi kwa uzalendo weledi, uadilifu na uaminifu hatua ambayo itaongeza kuleta tija kwa wafanyabiashara.

Kindamba aliyasema hayo katika ziara yake ya siku moja kutembelea Bandari ya Tanga,amesema lengo likiwa kujionea ufanisi utendaji mzuri unaofanywa na watendaji wakiongozwa na Meneja wao Masoud Mrisha.

Alisema, amefarijika na maboresho makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na fedha zilizotolewa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika bandari hiyo ambapo itakuwa lango la kufungua uchumi.

Alieleza,kuwa zaidi ya Bil 272 zimewekwa katika kufanya maboresho ya bandari ambapo maeneo kadhaa yameimarishwa ikiwemo ghati ambalo sasa inaruhusu Meli kubwa kuteremsha mizigo.

"Tumshukuru rais wetu Dk.Samia kwa umakini na utayari kuisaidia Bandari ya Tanga ili kuendelea kuwa shindani la kibiashara na bandari nyingine"alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga Kindamba.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tanga, amesema, anaitazama Bandari ya Tanga kama ya kimkakati zaidi na moyo wa uchumi ambapo ametembelea eneo hilo ili kuwatia moyo na faraja wafanyakazi na watumishi waendelee kuchapakazi.

Pamoja na kuyasema hayo, Mkuu huyo wa Mkoa ameelezea kuridhishwa kwake na bandari hiyo kuonekana kufanya kazi kwa mafanikio zaidi kila uchao ambapo kwa mara ya kwanza ilipokea Meli yenye urefu wa mita 150 na sasa siku aliyotembelea Meli yenye Mita 179 ilitia Nanga.

"Meli ya kwanza ilikuwa na Mita 150, leo bandari yetu imepokea Meli ya urefu wa Mita 179 haya ni mambo makubwa, pia Jumapili ijayo tutapokea Meli yenye ukubwa Mita 189.9 hivyo mambo yanazidi kuwa mazuri kwa Tanga"alisema.

Amewataka wakazi wa Tanga kuchangamkia fursa hiyo iliyoandaliwa na Serikali yao pia amewaomba wafanyabiashara ndani na nje nchi kuitumia Bandari ya Tanga.

Aidha,Mkuu huyo wa Mkoa alisema, kwa bandari ya Tanga usalama ni mkubwa,ufanisi ni wa hali ya juu huku akisema yuko tayari kushirikiana na wafanyabiashara na wadau mbalimbali.

Awali,Meneja wa Bandari ya Tanga,Masoud Mrisha  alisema amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga awasaidie kuwasukuma Tanroads na Tarura kutengeneza barabara ya kutoka bandari ya Tanga hadi Mwambani yenye urefu wa KM 7 ili kujengwa eneo la kuhifadhia mizigo.

Mrisha alisema,jambo jingine waliloliomba ni kutangazwa kwa bandari ya Tanga kwa kuita wakuu wengine wa mikoa na hata kuketi na wafanyabiasha wa mikoa ya Kaskazini ili kuona namna bora ya kutoa huduma.
Mwisho.



Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba, akiwa katika ziara ya kutembelea bandari ya Tanga mara baada ya kuzungumza na Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga.

 Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba, akiwa katika ziara ya kutembelea bandari ya Tanga mara baada ya kuzungumza na Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga akitembelea bandari hiyo.
Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Waziri Kindamba, akizungumza na waandishi wa habari bandari ya Tanga,akieleza mafanikio ambayo yatapatikana kwa wafanyabiashara na wananchi.

No comments:

Post a Comment