Pichani mkono wa kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Peter Milanzi akizungumza na waandishi wa habari ujio wa meli ya Mesovo yenye urefu wa Mita 190 ya mizigo iliyotokea Bandari ya Port Lake nchini Marekani mpaka kuwasili jijini Tangaakiwa na mkuu wa kitengo cha masoko Rose Tandika mkono wa kulia mwanamke.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MELI kubwa ya Mizigo inayofahamika kwa jina la Mesovo yenye urefu wa Mita 190 imetia nanga Bandari ya Tanga ikiwa ikiwa na mzigo wa Petcock wenye uzito wa tani 51,000.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Peter Milanzi amesema kuwa, meli hiyo mizigo imetokea Bandari ya Port Lake nchini Marekani mpaka kuwasili jijini Tanga.
Nae,Mkuu wa kitengo cha masoko Bandari ya Tanga,Rose Tandiko alisema kwamba tangu kukabidhiwa kipande cha ghati Bandari ya Tanga imekuwa ikivunja rekodi yake yenyewe.
"Leo tumepokea meli kubwa kuweza kuhudumia bandari ya Tanga MV Mesovo, kesho tutahudumia meli mbili"alisema Tandiko.
Pia ametumia nafasi hiyo kwa kuwataka wadau mbalimbali kufikiria kuitumia Bandari ya Tanga kwa maelezo kuwa utendaji wake umeimarika zaidi.
Naye,Seif Issa ambaye ni Meneja wa tawi Kampuni ya MR Instance Transporter ametoa wito kwa Wafanyabiasha kuwa tayari kuitumia Bandari ya Tanga, kwa madai kuwa iko Salama na hakuna mazingira yeyote ya utapeli kwa watumiaji.
Alisema kuwa Bandari ya Tanga wamejipanga, iko salama na huduma zote ziko vizuri ambapo aliwasihi wadau wengine kuitumia.
"Huduma ziko vizuri, kwa upande wetu wa Transporter hatujapata tatizo lolote, ufanisi umeongezeka zaidi"alisema Seif.
Wakala wa meli,Charles Cyprian nae alisema, katika utendaji Bandari ya Tanga imeimarika huku akisema wao kama wenyeji wa wenye meli siku ya kesho watapokea meli yenye tani 5500 za Amonium nitrate mzigo wa Simba Logistic.
Mwisho.

Pichani mwanamke ni Mkuu wa kitengo cha masoko bandari ya Tanga,Rose Tangika akizungumza na waandishi wa habari mkakati uliuopo kukaribisha wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi ili kuweza kuitumia kupitisha mizigo.
Picha ni Meli kubwa ya Mizigo inayofahamika kwa jina la Mesovo yenye urefu wa Mita 190 ikiwa imetia nanga bandari ya Tanga.
Pichani mkono wa kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Peter Milanzi ,katikati ni ,Mkuu wa kitengo cha masoko Bandari ya Tanga,Rose Tandiko mara baada ya mahojiano na waandishi wa habari kuzungumzia ujio wa meli hiyo na mikakati iliyopo kusaka masoko kukaribisha wafanyabiashara.
Pichani mkono wa kulia ni ,Meneja wa tawi Kampuni ya MR Instance Transporter,Seif Issa ambaye amevaa fulana nyeupe mara baada ya mahojiano na waandishi wa habari akiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo akieleza kwamba kampuni imejipanga kutoa huduma bora kwa wateja.
Pia ametoa wito kwa Wafanyabiasha kuwana utayari kuitumia Bandari ya Tanga, kwa madai kuwa iko Salama na hakuna mazingira yeyote ya utapeli kwa watumiaji.
No comments:
Post a Comment