Monday, 20 March 2023

ZOEZI LA USAILI WAREMBO WENYE SIFA KUWANIA TAJI LA MISS TANGA 2023 ILIKUWA HIVI,,

Pichani ni miongoni mwa warembo wakipata maelekezo ya kujiunga na shindano la Miss Tanga 2023 wakiwa kwenye usali wakipata maelekezo katka hafla ya uzinduzi jijini Tanga.

 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

MAANDALIZI ya Shindano la Miss Tanga 2023 yameendelea kushika kasi huku Wadau wakiahidi kushiriki bega kwa bega na Waandaaji ili kuwezesha shughuli hiyo kuwa ya aina yake.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa usaili wa warembo uliofanyika jijini Tanga,
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Monica Investiment yenye Saloon ya Wanawake  ambaye ni Miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo,Monica Swai.

Alisema, kwamba atatumia mashindano ya urembo ya mwaka huu kuwavutia wanawake kujitokeza ili kupata huduma ya kisasa.

Shindano hilo linatarajiwa kuwa la aina yake kutokana na maboresho amesema atahakikisha wanapata huduma bora na kuwezesha kuongeza ubora..

Alisema, wadau mbalimbali wameanza kujitokeza kuunga mkono shindano hilo akiamini kwamba watapatikana washiriki stahiki watakaoiwakilisha Tanga vizuri.

Mkurugenzi huyo wa kampuni ya Monica Investiment yenye Saloon ya Wanawake alisema kwamba sasa urembo ni fursa.

"Urembo ni fursa wasichana wasiogope kushiriki mashindano haya nawashauri wajitokeze kuchukua fomu"alisema Mkurugenzi huyo Monica.

Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Shaya Good Food Industry Ltd, Sekei Hassan alisema wamedhamiria kwa hali na mali kuunga mkono mashindano ya Miss Tanga 2023.

Sekei alisema, kampuni yake ambayo ni wazalishaji wa Vitafunwa 'snaks' imeamua kuingia kwenye soko kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Naye Mwakilishi kutoka kampuni ya African Star ambao ni wazalishaji na uuzaji nywele bandia nchini imeungana na waandaji kufanikisha shindano hilo la ulimbwende.

Tayari ratiba kwa ajili ya kambi kuanza imeshatoka ingawaje itatoa fursa kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuchukua nafasi yake.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment