Pichani ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe leo ofisini kwake akitoa taarifa mbalimbali za matukio ya uhalifu likiwemo lile la kuvunja Duka usiku na kuiba barabara ya nane jijini kwa mfanyabiashara maarufu fundi wa simu Omari.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA.
JESHI la Polisi Mkoani Tanga, limefanikiwa kuwakamata Watu nane (8) ambao wanaodaiwa kujihusisha na Vitemdo vya uhalifu wa uvunjaji ikiwa ni pamoja na unyang'anyi wa kutumia Silaha.
Katika Taarifa yake aliyoitoa leo kwa Vyombo vya habari Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga,Henry Mwaibambe alisema kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa kutoka kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo.

Alisema kwamba, mara baada ya kufanya tukio na kupata taarifa katika vituo vya polisi mkoani hapo ikiwemo cha Chumbageni jijini Tanga na kuunda timu,kuweka mtego maeneo mbalimbali ambapo ulifanikisha kuwanasa.
Aidha,alieleza kuwa baada watuhumiwa hao kukamatwa na kufanyiwa upekuzi kwenye makazi kule wanakoishi viliweza kupatikana vielelezo kadhaa ikiwemo Silaha aina ya Pistol yenye namba za usajili 007086.
Kamanda Mwaibambe alisema pia ilipatikana silaha yenye Magazine moja na risasi 10, ambapo ilikutwa huko Michungwani wilayani Handeni mkoani hapo.
Kamanda Mwaibambe alisema pia ilipatikana silaha yenye Magazine moja na risasi 10, ambapo ilikutwa huko Michungwani wilayani Handeni mkoani hapo.
Vielelezo vingine ni Pistol aina ya Colitm1911 A1 US ARMY ikiwa na Risasi mbili na ganda moja na Pistol iliyotengenezwa kienyeji isiyo na usajili.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe alisema silaha nyingine zilikamatwa Kata ya Tangasisi iliyopo kwenye Halmashauri ya Jiji laTanga.
Kamanda Mwaibambe aliwataja waliokamatwa kuwa ni Akida Abushiri maarufu kama bichwa ambaye ni mkazi wa Mikanjuni na Dickson Mayunga (45) mkazi wa Kwalubuye Muheza.
Wengine wanaoshikiliwa ni Ally Abdallah (37) wa Michungwani Handeni, Hussein Bakari Mtambo (37) wa Bwitini Muheza na Salimu Riziki wa Usagara Jijini Tanga.
Watuhumiwa wengine ni Edward Allen Gosi (23) nb Ally Mustapher (25) wote wa Usagara Tanga ambapo watafikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria kuweza kuchukua mkondo wake.

Pia pia katika msako uliofanywa na jeshi la polisi wamefanikiwa kukamata simu 18 aina ya Smart phone,Television 4 na pikipiki nane.
''Uhalifu huo ukiwemo tukio la kuvunja duka usiku na kuiba eneo la baraba ya nane jijini Tanga kwa mfanyabiashara maarufu fundi wa simu Omari''alisema Kamanda Mwaibambe.
Mwisho.
Mwisho.
Pichani katikati ambaye anaongea ni Kamanda wa JPolisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe jana ofisini kwake akitoa taarifa kwa waandishi wa habari akiwa na baadhi ya maofisa wengine wa jeshi la polisi mkoani hapo.
Pichani wa kwanza kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe leo ofisini kwake akitoa taarifa kwa waandishi wa habari akiwa na baadhi ya maofisa wengine wa jeshi la polisi mkoani hapo.
No comments:
Post a Comment